Monday, 16 November 2015

Mkwasa: nitashinda mapema Algeria

Mkwasa: nitashinda mapema Algeria

Tarehe November 16, 2015

.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa amesema atahakikisha timu yake inapata ushindi wa mapema katika mchezo wa marudiano dhidi ya Algeria utakaochezwa kesho.

Stars imeondoka jana usiku nyuma ya Algeria mara baada ya mchezo huo kumalizika kuelekea nchini Algeria tayari kwa ajili ya marudiano.

 Mkwasa alisema kuwa sasa nguvu zake anazielekeza katika mchezo huo ili kuhakikisha wachezaji wake wanatengeza nafasi na kuzitumia ipasavyo ili kupata ushindi wa mapema.

Alisema kwa sasa anaimani kubwa na kikosi chake kutokana na  mchezo mchezo waliouonesha katika uwanja wa Taifa.
Alisema kuwa kwa kuwa hakuna muda wa kupumzika na wa mazoezi magumu atahakikisha anatumia muda uliopo ili kuondoa kasoro zilizowakosesha magoli katika mchezo wa awali.

“Kikubwa ni kutengeneza nafasi na kuhakikisha tunazitumia ipasavyo ili kuweza kuondoka na ushindi wa mapema kwani tutahakikisha tunapambana zaidi ya tulivyopambana Taifa”, alisema Mkwasa.

Akizungumzia mchezo uliopita Mkwasa alisema kuwa ni kweli kuwa mabadiliko aliyoyafanuya kipindi cha pili yalikuwa na makosa yaliyopelekea Algeria kurudisha magoli na mchezo kuisha kwa sare ya 2-2.

Alisema, lengo la kufanya mabadiliko ni kuongeza nguvu na kasi ya mchezo lakini kwa bahati mbaya ilikuwa kinyumena matarajio yao.

“Wachezaji wetu wamecheza vizuri ila tulifanya makosa kwa kufanya mabadiliko kwasababu timu ilikuwa inaongoza lakini mchezo ndivyo ulivyo na nafikiri bado tuna safari mbele yetu na ninavyowatazama hawa nyumbani kwao watabadilika”, alisema Mkwasa.

Mkwasa alisema kuwa watanzania waendelee kuwa na imani kwani Algeria wanafungika na sivyo kama walivyokuwa wakiwasikia kuwa ni timu ngumu kutokana na wachezaji wake 18 wanaounda kikosi hicho kuchezea barani Ulaya.

clouds stream