Wednesday, 25 November 2015

Waziri mkuu akerwa kusuasua Mabasi yaendayo kasi


Waziri mkuu akerwa kusuasua Mabasi yaendayo kasi

Tarehe November 25, 2015

Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amekerwa na kusua sua kwa mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi  licha kuwa mabasi kadhaa yalianza kufanya kazi siku kadhaa zilizopita jijini Dar es salaam.
Kutokana na kusua sua huko  ambako hakuendani na kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ Majaliwa ameitisha kikao ofisini kwake leo saa 4 asubuhi akitaka kupatiwa taarifa ni kwa nini mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) haujaanza kazi hadi sasa.
“Ninataka kupata haya maelezo kwa sababu Watanzania na hasa wana-Dar es salaam, wamesubiri kwa muda kuona mradi ukianza kazi ili uondoe kero ya usafiri. Wao wanajua anayehusika ni TAMISEMI,”aliongeza.

Watakao jieleza mbele ya Waziri mkuu ni Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mkuu DART na watendaji wake wote pamoja na watu wengine wanaohusika katika utekelezaji mradi huo.
Baaada  ya kujieleza watatakiwa  kutoa majibu ya lini  Mabasi hayo yataanza kazi, je ni nani anakwamisha na hata kama ni sheria, ni kwa nini wasitafute namna  kuondoa hivyo vikwazo.

clouds stream