Tuesday, 10 November 2015

Chama kipya cha Siasa chaanzishwa nchini

Chama kipya cha Siasa chaanzishwa nchini

Tarehe November 10, 2015
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini amewataka  viongozi wa chama kipya  cha siasa nchini Tanzania  cha Tanzania Patriotic Front (TPF-Mashujaa) kuzingatia  Katiba na sheria ya vyama vya siasa.
Akizungumza  ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Mutungi alisema kumekuwa na ongezeko la vyama vya kisiasa nchini na wengine wameanzisha kama mchezo wa kuigiza, wanafanya udanganyifu na kukiuka Sheria, Katiba na Kanuni za vyama vya siasa.
Amewapongeza waasisi wa chama kipya cha kwa dhamira yao ya dhati kwa kuanzisha chama baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa kuwa  wameonesha wana  dhamira ya dhati ya kuanzisha chama kitakacholeta mabadiliko.
Mmeacha uchaguzi upite, maana ingekuwa mnataka madaraka pekee, mngeanza kabla ya uchaguzi,” alisema Jaji Mutungi kabla ya kukabidhi cheti cha usajili wa muda kwa waasisi hao, Denatus Mutani na Optatus Likwelile.
Nao, waanzilishi wa chama hicho, Mutani (Mwenyekiti wa muda) na Likwelile (Katibu wa muda), waliahidi kwa nyakati tofauti kuwa watasimamia ipasavyo sheria na kanuni za usajili pamoja na Katiba ya nchi. Chama hicho kimedai kinalenga kuwaelimisha Watanzania kuwa siasa ni maisha badala ya kudhani kuwa lengo ni kushika madaraka fulani pekee.
Msajili alisema kutokana na usanii wa kuanzisha vyama kiholela mpaka sasa kuna vyama 22 vyenye usajili wa kudumu nchini na vingine kadhaa visivyo na usajili.

clouds stream