Friday, 29 April 2016

EPL Leo Arsenal Dimbani Na Norwich City

EPL Leo Arsenal Dimbani Na Norwich City

Tarehe April 29, 2016
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akiwa na mshambuliaji wake Olivier Gioud
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akiwa na mshambuliaji wake Olivier Gioud
Ligi kuu ya soka ya England inaendelea tena hapo kesho kwa michezo kadhaa,Everton ni wenyeji wa Bournemouth, Newcastle United wanawaalika Cristal Palace,Stoke city dhidi ya,Sunderland,Watford watachuana na Aston Via,West Brom wanawaalika West Ham United, na Arsenal watakuwa wenyeji wa Norwich city.
Hadi sasa ligi hiyo inaongozwa na Leicester city yenye alama 76,Tottenham alama 69,Man city alama 64 sawa na Arsena yenye alama 64.
Katika nafasi ya mwisho katika msimamo Timu za Aston via na Newcastle ndio Timu zinazoburuza mkia kufuatia kuwa na alama chache kuliko Timu zote,Idhaa ya Kiswahili ya BBC itakutangazia mechi kati ya New castle Unite na Cristal palace.

Panga Pangua Ya Kamati Za Bunge Yawakera Wabunge

Panga Pangua Ya Kamati Za Bunge Yawakera Wabunge

Tarehe April 29, 20161
1
Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko mengine ya kamati za Bunge kwa kuwaongeza wabunge wapya na kuwahamisha wengine kwenda kwenye kamati nyingine, jambo ambalo limepingwa na baadhi ya wabunge wakidai linapunguza ufanisi.
Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Bunge, mabadiliko hayo yamefanyika kwa mujibu wa kanuni ya 116 (3) na (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2016, ili kuhakikisha kila mbunge anakuwa mjumbe wa kamati mojawapo ya Bunge.
Juzi, Kwa mara ya pili, Spika Ndugai aliwaongeza wabunge wanne wapya walioapishwa bungeni Aprili 19, kwenye kamati za Miundombinu; Ardhi, Maliasili na Utalii; Kilimo, Mifugo na Maji; na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), alisema mabadiliko hayo yanaonyesha namna ambavyo Spika Ndugai ‘anavyokosa umakini katika uundaji wa kamati hizo’.
Naye Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM) alisema mabadiliko yanayofanywa hayawezi kuleta tija katika bunge hilo, kwani watu wanashindwa kujipanga vyema kwa kuwa hawajui kesho itakuwaje.

Naibu Spika Azua Gumzo Kwa Kumuita Mbunge ‘ Bwege’

Naibu Spika Azua Gumzo Kwa Kumuita Mbunge ‘ Bwege’

Tarehe April 29, 2016
Naibu Spika wa Bunge  Tulia Ackson.Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson.                                                                       Naibu Spika Tulia Ackson amezua gumzo Bungeni jana  kufuatia  kumuelezea mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Said Bungara kuwa ni bwege.
 “Na wewe Mheshimiwa Bwege, hebu kaa chini. Usionyeshe ubwege wako hapa,” alisema Dk Ackson kumzuia mbunge huyo asiendelee kuzungumza wakati  wa mjadala.
Kitendo cha kutumia neno bwege kumuelezea mbunge huyo kilisababisha wapinzani wacharuke, na kuibua bungeni kesi ya mtu aliyefunguliwa mashtaka mkoani Arusha kwa kosa la kumuelezea Rais John Magufuli kuwa ni bwege.
Bila ya kuruhusiwa, mmoja wa Wabunge  alifungua kipaza sauti na kusema: “Hatimaye msamiati wa bwege watua bungeni sasa kutumika rasmi. Futa lugha ya kuudhi; bwege bwege.”
Akizungumzia suala hilo Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Antony Komu alisema: “Kauli iliyotolewa na Naibu Spika inaonyesha wazi kuwa ni kiongozi anayekiuka misingi, taratibu na kanuni za Bunge. Tazama anatukana watu tu bila kujali jambo lolote, hii si sawa kabisa.”
Naye Mbunge wa Kalenga (CCM), Godfrey Mgimwa alisema Dk Tulia alighafilika wakati akitoa kauli hiyo baada ya kurushiwa maneno mara kwa mara na wabunge wa upinzani, tena bila kufuata kanuni na taratibu za kibunge.
Hivi karibuni  Mkazi wa  Arusha, Isaack Habakuk Emily alipandishwa kizimbani  akikabiliwa na shitaka la kumuita Rais kuwa ni bwege.

Tuesday, 26 April 2016

Kina Ronaldo Washatua Manchester City Ona Picha

Kina Ronaldo Washatua Manchester City Ona Picha

Tarehe April 26, 2016Ronaldo akiwa ndio anatoka katika lango la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Manchester city
Ronaldo akiwa ndio anatoka katika lango la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Manchester city
Ronaldo akiwa ndio anatoka katika lango la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Manchester city
Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hatua ya Nusu fainali inaendelea tena leo ambapo Manchester City watamenyana na Real Madrid,Kikosi cha Real Madrid kimetua katika jiji la Manchester City kukabiliana na wenyeji wao Manchesetr City
katika Mechi hiyo Man City wanatakuwa na pigo kubwa la kumkosa Kiungo wao kutoka Ivory Coast, Yaya Toure.
nimekuwekea Picha za Real Madrid walipokuwa wakiwasili Manchester13076997_10151027070059953_7346205144108414913_nSergioa Ramos naye alipata wasaha wa kuongea na mashabiki
13076997_10151027070059953_7346205144108414913_n
Sergioa Ramos naye alipata wasaha wa kuongea na mashabiki
Sergioa Ramos naye alipata wasaha wa kuongea na mashabikiRonaldo kama kawaida yake ni kipenzi cha mashabiki

Ronaldo kama kawaida yake ni kipenzi cha mashabiki
Ronaldo kama kawaida yake ni kipenzi cha mashabikiPepe akiongea na mashabiki

Pepe akiongea na mashabiki
Pepe akiongea na mashabikiGareth Bale akisalimiana na mashabiki walifika kuwapokea
Gareth Bale akisalimiana na mashabiki walifika kuwapokea
Gareth Bale akisalimiana na mashabiki waolifika kuwapokea

Mkurugenzi Mkuu TCRA Na Bodi Yake Watumbuliwa

Mkurugenzi Mkuu TCRA Na Bodi Yake Watumbuliwa

Tarehe April 26, 2016Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS), na hivyo kuisababishia nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo baada ya kufanya kikao kazi kati yake na uongozi na wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Rais Magufuli pamoja na kuchukua hatua hizo, amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo maramoja.
Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri wa Mawasiliano Makame Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika Wizara hiyo kuchukua hatua maramoja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi nan chi iweze kupata mapato yanayostahili kukusanywa.
“Waziri hakikisha unachukua hatua maramoja, nataka tukusanye mapato yote ya Serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua dhidi ya yeyote atakayekwamisha jambo hili,” amesisitiza Rais Magufuli.
Mnamo Mchi 22, 2013, TCRA iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekezaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambayo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na udhibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha Serikali kukosa mapato ya kiasi hicho cha fedha kilichotajwa.

Friday, 22 April 2016

Picha : Ona Mashabiki Wa Arsenal Walivyosusia Mechi Kisa Mzee Wenger

Picha : Ona Mashabiki Wa Arsenal Walivyosusia Mechi Kisa Mzee Wenger

Tarehe April 22, 2016Arsenal-fans-1-1

Arsenal-fans-1-1
Picha inaonyesha mashabikiwa Arsenal wakiwa pungufu sana uwanjani
Timu ya Arsenal ilijikuta katika wakati mgumu ambapo katika uwanja wa Emirates usiku wa Alhamisi wakati Arsenal Ikicheza dhidi ya West Brom ambapo uwanja mashabiki wengi wa Arsenal hawakujitokeza uwanjani kushuhudia mchezo huo kama ilivyo kawaida yao.
Arsenal-fans-2

Arsenal-fans-1
 Arsenal-fans-2
 Arsenal-fans-1

Asilimia 79 Ya Simu Zinazotumiwa Na Watanzania Ni Halali


Asilimia 79 Ya Simu Zinazotumiwa Na Watanzania Ni Halali


Tarehe April 22, 2016
1
meneja uhusiano wa TCRA, Innocent Mungi
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa asilimia 79 ya simu za kiganjani zilizofanyiwa utafiti kwa kipindi cha desemba hadi February mwaka huu ni halali, huku asilimia 18 zikionekana zikiwa za bandia.
Akizungumza katika semina ya mfumo wa rajisi ya  namba za utambulisho wa simu za kiganjani, meneja uhusiano wa TCRA, Innocent Mungi amesema kutokana na elimu ambayo wameitoa kwa wafanyabiashara wa simu  hizo ya kuhakiki kwanza kabla ya kuwauzia wananchi imepunguza uingizaji wa simu feki na kwamba wamebaini kuwa asilimia 79 ni salama hazina matatizo ya aina yeyote.
“Wakati tumeanza kubaini zoezi la kutambua simu feki tulibaini kuwa asilimia 30 zilikuwa bandia ila kutokana na elimu iliyotolewa hadi February simu bandia zimepungua hadi kufikia asilimia 18 hii inaonyesha kuwa simu feki zilizoko sokoni ni chache mno,” aliongeza.
Aidha, Mungi alitaja faida za kuzimiwa simu bandia kuwa ni pamoja na kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu ,kupunguza wizi wa simu  na kupunguza matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitumika mara nyingi kwa njia ya simu hizo pamoja na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango.
Awali mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Ally Simba aliwataka wananchi kufanya zoezi la kuhakiki simu zao kwa kufuata maelekezo sahii ili waweze kubaini simu feki kabla ya kuzimiwa simu hizo juni 16 ,kwani wengi wa watumiaji wa simu hawafuati malekezo ya kutambua simu bandia.

Serikali: Rais Hawezi Kujipunguzia Mshahara

Serikali: Rais Hawezi Kujipunguzia Mshahara

Tarehe April 22, 2016Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Suala la mshahara wa Rais, limeibuka tena bungeni ambapo Bunge limeelezwa kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais hawezi kujipunguzia mshahara pindi anapoapishwa kushika wadhifa huo.
Akitoa taarifa kwa Bunge, Waziri Simbachawene alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake, Ibara ya 43, Ibara ndogo ya 3, Ukurasa wa 62 inamzuia Rais kupunguza mshahara akiwa madarakani.
Simbachawene alisema ibara hiyo inasema;  ‘Mshahara na malipo ya Rais, havitapunguzwa wakati Rais anapokuwa bado anashika madaraka yake. “Rais aliyepo sasa hawezi kujipunguzia mshahara wake yeye mwenyewe isipokuwa anapoondoka anaweza kuweka kiwango cha mshahara cha Rais ajaye.
Simbachawene alitoa maelezo yake akimjibu Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema) aliyemuomba Rais John Magufuli kujipunguzia mshahara na kuanza kulipa kodi.
Akiwa nyumbani kwake Chato mkoani Geita wakati alipokwenda kwa mapumziko mafupi hivi karibuni, Rais Magufuli alijitangazia mbele ya umma kiwango cha mshahara anacholipwa akisema ni Sh milioni 9.5 kwa mwezi.

Daladala Zatakiwa Kupotea Katikati Ya Jiji Ifikapo Mei 2

Daladala Zatakiwa Kupotea Katikati Ya Jiji Ifikapo Mei 2

Tarehe April 21, 2016
Daladala zote zinazofanya safari zake katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam zimetakiwa kuwa zimeondoka iikapo Mei 2, mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (DART), Sabri Mabrouk ambaye amedai ya kuwa tayari wamiliki wote wa mabasi hayo wamekwishalipwa fidia ili wabadili njia zao za usafiri nje ya katikati ya Jiji.
“Wamiliki wote wa mabasi wamekwishalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana na sasa hakuna yeyote anayedai hivyo wana siku saba tu kuhakikisha kuwa wamekwishaondoka katika barabara hizo kabla ya Mei 10,” amesema Mabrouk ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (DARCOBOA).
Tayari mabasi yaendayo kasi yamekwishaanza majaribio ya kupita katika njia zake huku huduma hizo zikitarajiwa kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu.

Monday, 18 April 2016

Matokeo Mechi Zote Za Jana Angalia Hapa,Msimamo Wa Ligi Pia


Matokeo Mechi Zote Za Jana Angalia Hapa,Msimamo Wa Ligi Pia


Tarehe April 18, 2016Jamie Vardy
Jamie Vardy
Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL kufikia 18 Aprili, 2016.
NambariKlabuMechiMabaoAlama
1Leicester342673
2Tottenham333565
3Man City332860
4Arsenal332260
5Man Utd331056
6West Ham331253
7Southampton341051
8Liverpool32951
9Stoke33-647
10Chelsea33444
11Everton33941
12Watford33-541
13Bournemouth34-1641
14West Brom33-940
15Swansea34-1140
16Crystal Palace34-739
17Norwich34-2531
18Sunderland33-1830
19Newcastle33-2628
20Aston Villa34-4216

Bournemouth1-2Liverpool
Leicester City2-2West Ham United
Arsenal1-1Crystal Palace

Friday, 15 April 2016

Liverpool Noma Waitoa Dortmund Europa

Liverpool Noma Waitoa Dortmund Europa

Tarehe April 15, 2016
TimuJurgen Klopp akishangilia
Jurgen Klopp akishangilia
Jurgen Klopp akishangilia
za Liverpool, Shakhtar Donetsk na Villarreal zimetinga Nusu Fainali ya michuano ya Europa League 2016 baada ya mechi za marudiano usiku wa Alhamisi.
Liverpool imesonga mbele baada ya kuifunga 4-3 Borussia Dortmund Uwanja wa Anfiled, hivyo kufuuz kwa ushindi wa jumla wa 5-4 baada ya wiki iliyopita kutoa sare ya 1-1 Ujerumani.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Divock Origi dakika ya 48, Philippe Coutinho dakika ya 66, Mamadou Sakho dakika ya 77 na Dejan Lovren dakika ya 90 na ushei, wakati ya Dortmund yamefungwa na Henrikh Mkhitaryan dakika ya tano, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya tisa na Marco Reus dakika ya 57.
Shakhtar Donetsk imeifunga 4-0 Sporting Braga na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-1 baada ya awali kushinda 2-1 ugenini. Mabao ya Shakhtar yamefungwa na Darijo Srna kwa penalti dakika ya 25, Ricardo Jose Araujo Ferreira aliyejifunga dakika ya 42 na 73 na Viktor Kovalenko dakika ya 50 Uwanja wa Lviv.
Villarreal imeshinda 4-2 ugenini dhidi ya Sparta Prague na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-3, baada ya wiki iliyopita kushinda 2-1 nyumbani.
Sevilla imeing’pa Athletic Club ka penalti 5-4 kufuatia sare ya jumla ya 3-3, baada ya kila timu kushinda 2-1 mechi ya nyumbani.

Mradi Wa DART Sasa Kuanza Mei 10

Mradi Wa DART Sasa Kuanza Mei 10

Tarehe April 15, 2016
10262227_717689465039977_2529648417247638500_n
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, George Simbachawene amesema mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) utaanza rasmi Mei 10, mwaka huu wakati akifanya majumuisho ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
Simbachawene amesema kuwa wadau wa mradi huo wamemhakikishia kuwa mabasi hayo yataanza kutoa huduma ya usafiri ifikapo Mei 10 baada ya kukutana nao na kuzungumza kwa kirefu.
“Tumeambiwa kuwa mradi huu una mikataba mingi na kwamba bado kuna majadiliano makubwa ya mikataba hivyo hatuwezi kulazimisha maana unaweza kujikuta ukitengeneza mikataba mibaya na tunaendelea na mijadala ya mikataba hiyo ingawa uwazi ni muhimu sana,” amesema.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawalana Serikali za Mitaa, Jasson Rweikiza amesema kamati yake imeshatembelea mradi huo zaidi ya mara nne na kugundua tatizo linalokwamisha ni fedha na kuitaka Serikali kuhakikisha inatoa fedha ili huo uanze mara moja kama ilivyokusudiwa.
Amesema ni muhimu sana kwa mradi huo kukamilika na kuanza kutoa huduma maramoja ili kupunguza kero ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaoteseka na tatizo la usafiri na foleni za barabarani.

Kigogo Aikacha Chadema Amfuata Magufuli CCM

Kigogo Aikacha Chadema Amfuata Magufuli CCM

Tarehe April 15, 2016
Chadema
Chadema
Kigogo wa Chama cha Demokrsaia  na Maendeleo (Chadema) ambaye alikuwa  Mwenyekiti wa chama mkoa wa Mwanza   Andrian Tizeba ametangaza kuhamia Chama  cha Mapinduzi (CCM).
Aidha, Bw.Adrian  leo amejiunga rasmi na CCM wilayani  Sengerema tawi la Lugata  ambapo  alitangaza kujivua uanachama wa chadema Machi 29 mwaka huu baada ya kusimamishwa uongozi kwa muda wa mwaka mmoja, na kutangaza kuachana na siasa, amekabidhiwa kadi hiyo  na katibu wa tawi hilo Alfred Mwambala.
Kwa upande wake Tizeba amesema uamuzi wake si wa kulazimishwa na mtu bali, ameona ni vema arudi kwenye chama chake cha awali   kutokana na kuridhishwa na  utendaji wa Rais Dkt.  John Magufuli.

Kampuni Ya Infosys Yaikana Vikali Lugumi Enterprises

Kampuni Ya Infosys Yaikana Vikali Lugumi Enterprises

Tarehe April 15, 2016infosys
infosys
Kampuni ya Infosys  IPS (T) Ltd, imejitokeza na kukanusha vikali taarifa zinazoendelea katika mitandao ya kijamii zikiihusisha kampuni hiyo na kampuni ya Lugumi Enterprises inayokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu na mkataba mbovu baina yake na Jeshi la Polisi.
Naibu Meneja Mkuu wa Infosys, Sweki Donald amesema kuwa kampuni hiyo haijawahi kufanya biashara yoyote na kampuni tajwa ya Lugumi Enterprises na kusisitiza kuwa kampuni hizo mbili hazina mahusiano yoyote yale ya kibiashara.
Tangu kuibuke kwa kashfa ya mkataba tata kati ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi juu ya ufungwaji wa mashine za kutambua alama za vidole katika vituo vya polisi nchi nzima, kumekuwa na habari zinazosambaa kuwa kampuni ya Infosys ilipokea mabilioni ya shilingi kutoka kampuni ya Lugumi, jambo ambalo wanadai kuwa halina ukweli wowote na kutoa rai kwa umma kupuuza taarifa hizo za upotoshaji.
Katika mkataba huo wa mwaka 2011, Kampuni ya Lugumi Enterprises ilipewa tenda ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini kwa gharama ya Sh bilioni 37.
Tayari kampuni hiyo imekwishalipwa Shilingi bilioni 34 sawa na asilimia 99 ya fedha zote, huku ikiwa imefunga mashine katika vituo 14 tu katika jiji la Dar es Salaam ambavyo pia havijulikani vipo maeneo gani.

Tuesday, 12 April 2016

Picha Azam Fc Wakijifua Jioni Ya Leo


 Picha Azam Fc Wakijifua Jioni Ya Leo


Tarehe April 11, 2016Mwantika akipiga mbizi ilikuweka mwili safi
Mwantika akipiga mbizi ilikuweka mwili safi
Mwantika akipiga mbizi ilikuweka mwili safi
Baadhi ya wachezaji wa Azam FC walivyofanya mazoezi binafsi mara baada ya mazoezi ya jioni ya leo, mabeki David Mwantika na Gadiel Michael walikuwa wakifanya mazoezi ya kutafuta pumzi ndani ya bwawa la kuogelea kwa kuzama chini na kupiga mbizi kinyumenyume na kwa kwenda mbele.
12957438_1165368266836861_1295259493603279876_oWinga Khamis Mcha yeye alitumia muda wake binafsi kufanya mazoezi ya ‘gym’, yote hayo ni katika kujiweka fiti zaidi kimwili.12973350_1165368323503522_8479810840086730883_o
12973350_1165368323503522_8479810840086730883_o

 12985366_1165368180170203_2814174795365792906_n
12957438_1165368266836861_1295259493603279876_o
12985366_1165368180170203_2814174795365792906_n
12983309_1165368446836843_2723698762222629130_o12983309_1165368446836843_2723698762222629130_o

clouds stream