Mkulima mmoja wa Kitongoji cha Upangwani Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata ya Masanze JImbo la Mikumi Morogoro aliyepigwa mkuki.(Tahadhari Picha zinatisha)
Migogoro ya Wakulima na Wafugaji isiyokwisha Mkoani Morogoro imepelekea mkulima aliyejulikana kwa jina la Augustino Mtitu kupigwa mshale mdomoni na kutokea shingoni na Mfugaji wa Kimasai jana.
Kwa mujibu wa tarifa ya Katibu Ofisi ya Mbunge Prof. Jay Bw. Robert A. Galamona imebainisha kuwa Kijana huyo Augustino Mtitu alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa akimsaidia jirani yake kufukuza Ng’ombe wasiharibu mazao shambani kwake.
Mkulima huyo kwa alikimbizwa hospitali ya wilayani Kilosa na baadae alipelekwa hospitali ya mkoa Morogoro ili kufanyiwa operesheni ya kuondoa mkuki huo na matibabu zaidi.
Aidha, Kipande cha mti kinachoonekana (pichani) mdomoni ndiyo mkuki uliokatwa ili kupunguza urefu wa mkuki huo wakati wakimkimbiza hospitali, Inasemekana MwenyeKiti wa kijiji na MwenyeKiti wa kitongoji hicho nao wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Ofisi Ya Mbunge Mikumi, Profesa Jay imetoa wito kwa Serikali kuwabaini wale wote waliofanya kitendo hiki cha kinyama kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia sheria mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu mkubwa wa Amani na migogoro isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa.
Mkuliwa aliyepigwa mshale mdomoni na kutokezea Shingoni
Mkulima huyo akipelekwa Hospitali.