Wednesday 28 December 2016

Yanga Wailaza Ndanda 4-0 Shamba La Bibi

Domald Ngoma akiwahi kuupiga  mpira mbele ya beki wa Ndanda, Bakari Mtama uwanja wa uhuru Dar es salaam.
Domald Ngoma akiwahi kuupiga mpira mbele ya beki wa Ndanda, Bakari Mtama uwanja wa uhuru Dar es salaam.
img-20161130-wa0008

Klabu ya Yanga leo imejipatia pointi tatu muhimu baada ya kuifunga Ndanda ya Mtwara mabao 4­0 katika mchezo wa ligi kuu Vodacom uliochezwa uwanja wa Uhuru jijini Dares salaam.

Kufuatia ushindi huo Yanga SC inafikisha pointi 40 ikizidiwa pointi moja na watani wao, Simba SC ambao kesho watacheza na klabu ya Ruvu Shooting.

Katika mchezo huo Mshambuliaji Donald Dombo Ngoma alifunga mabao mawili mfululizo, Amissi Joselyn Tambwe alifunga bao la tatu na beki Mtogo, Vincent Bossou akafunga la nne kipindi cha pili.

clouds stream