Wednesday, 28 December 2016

Netanyahu aipinga hotuba ya Kerry kuhusu makazi

Ujenzi wa Makaazi ya Wayahudi

Ujenzi wa Makaazi ya Wayahudi
img-20161130-wa0008

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani John Kerry ameutetea uamuzi wa nchi yake wa kuliwezesha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuupitisha uamuzi wa wiki iliyopita, kutangaza Makazi ya Wayahudi kuwa ni kitendo kilicho kinyume na sheria.

Waziri Kerry amesema hatua hiyo ina nia ya kulinda uamuzi wa kuwepo kwa mataifa mawili ili kuzuia hatari ambayo ingeweza kutokea.

Amesema bila ya usalama wa Israel na uwepo wa Palestina, Israel hakutakuwa na amani kamili.

Lakini hata hivyo, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea kuvunjwa moyo na hotuba iliyotolewa na John Kerry kuhusiana na jambo hilo, ambayo ameielezea kuwa haijakaa sawa.

Amesema ukweli ni kwamba Wapalestina wamekataa kukubali uwepo wa Israel.

Kwa upande wake, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema atakuwa tayari kurudi katika mazungumzo pale tu Israel itakapoacha kujenga makaazi  mapya ya wananchi wake katika eneo la Wapalestina.

clouds stream