Friday, 9 December 2016

Wabunge wapiga kura kumfuta rais wa Korea Kusini Park Geun-hye

Waandamanaji wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Seoul wakutaka Bi Park aondolewe madarakani

Waandamanaji wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Seoul wakitaka Bi Park aondolewe madarakani
img-20161130-wa0008

Wabunge nchini Korea Kusini wamepiga kura kumuondoa madarakani Rais wa Park Geun-hye.

Hoja hiyo imepitishwa na wabunge 234 dhidi ya 56.

Maelfu ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Seoul wakitaka Bi Park aondolewe madarakani.

Hatua hiyo itamlazimisha Bi Park kung'atuka kwa muda huku Mahakama ya Kikatiba ikiamua iwapo ataondolewa kabisa kutoka wadhifa huo wa urais.

Suala kuu limekuwa ni uhusiano kati ya Bi Park na msiri wake mkuu Choi Soon-sil, ambaye anadaiwa kutumia uhusiano huo kujizolea ushawishi nchini humo.

Viongozi wa mashtaka wanasema Bi Park alikuwa na "mchango mkubwa" katika visa kadha vya ufisadi, tuhuma ambazo amezikanusha.

Aidha, alikataa wito wa kumtaka ajiuzulu akisema uamuzi huo aliuachia bunge.

Bi Park amekataa wito wa kumtaka ajiuzulu
Bi Park amekataa wito wa kumtaka ajiuzulu
img-20161130-wa0008

Bunge la Korea Kusini lilianzisha hoja hiyo Alhamisi, ambapo iilihitaji kuungwa mkono na angalau theluthi mbili ya wabunge ndipo kupitishwa.

Wachanganuzi walikuwa wanasema hilo lingekuwa jambo ngumu.

Bunge linatawaliwa na vyama vya upinzani na wabunge huru ambao wanataka aondolewe madarakani, lakini walihitaji wabunge 28 zaidi kutoka kwa chama cha Saenuri, chake Bi Park, ndipo wafikishe idadi ya kura inayohitajika.

Lakini matokeo yanaonesha wapo wabunge wa chama chake waliompinga.

Choi Soon-sil
Bi Choi ni rafiki wa karibu wa Bi Park

clouds stream