Wednesday 14 December 2016

Kanye West akutana na Donald Trump New York

Donald Trump na Kanye West wakitabasamu

img-20161130-wa0008

Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Kanye West, ambaye majuzi alilazwa hospitalini baada ya kutatizwa na msongo wa mawazo na uchovu, amekutana na rais mteule wa Marekani Donald Trump jijini New York.

Bw Trump anasema wawili hao walizungumza kuhusu "maisha" kabla ya kupigwa picha pamoja.

Alisema wawili hao ni "marafiki" na akamweleza Kanye kuwa "mtu mzuri" lakini hakusema iwapo mwanamuziki huyo atatumbuiza wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake mwezi Januari

Kanye alisalia kimya alipokuwa na mwanachama huyo wa Republican.

Aliwaambia wanahabari: "Nataka tu kupigwa picha kwa sasa."

Taarifa kutoka Marekani zinasema Bw Trump huenda anakabiliwa na tatizo katika kutafuta wanamuziki mashuhuri wa kutumbuiza siku ya kuapishwa kwake.

Kanye West akiwa Trump TowersTrump Tower ndiyo makao makuu ya The Trump Organisation, kampuni inayomiliki biashara za rais huyo mteule.

Kanye amekuwa akipumzika na kupata nafuu kutokana na matatizo ya kiafya aliyoyapata mwezi jana.

Mwaka uliopita, Kanye alitangaza kwamba anakusudia kuwania urais mwaka 2020.

Lakini hivi majuzi alisema iwapo angepiga kura uchaguzi wa mwaka huu, basi angempigia Donald Trump.

"Niliwaambia kwamba sikupiga kura," aliwaambia mashabiki San Jose, California. "Lakini sikuwaambia... iwapo ningepiga kura, kwamba ningempigia kura Trump."

Tangu ashinde urais, ulinzi umeimarishwa Trump Tower, jumba ambalo rais huyo mteule amekuwa akitumia kama afisi.

Haijabainika Kanye West na Donald Trump walizungumzia nini wakati wa mkutano huo.

Donald Trump and Kanye WestMapema Jumanne, Bw Trump alitangaza kwamba atamteua afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya mafuta ya Exxon Mobil, Rex Tillerson, kuwa waziri wake wa mambo ya nje.

clouds stream