Monday 5 December 2016

Urusi na China walipinga Baraza la Usalama kuhusu Aleppo

Wanajeshi nchini Syria

Majeshi nchini Syria
img-20161130-wa0008

Urusi na China wamepiga kura ya turufu kupinga mapendekezo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na kusitishwa mapigano siku saba katika mji wa Aleppo, ili kupisha uingizwaji wa misaada ya kibinadamu.

Kutokana na msimamo huo, Marekani imesema kuwa Urusi inalenga kulinda maslahi yake ya kijeshi, badala ya kuwasaidia raia wa mji huo wa Aleppo.

Naye balozi wa Urusi katika Umoja wa mataifa Vitaly Churkin, amesema hatua hiyo ya kusitisha mapigano itasababisha waasi kujipanga upya.

"Kama tunavyofahamu, aina hii ya usitishaji mapigano imekuwa ikisababisha waasi hawa kujipanga na kupata nguvu tena. Kwani kuwaacha wakiwa wanashikilia baadhi ya maeneo ndiko kusaidia raia?" ameuliza Churkin.

Hii ni mara ya sita ndani ya miaka mitano, Urusi imeweza kutumia kura yake ya turufu kupinga mapendekezo ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kuhusiana na vita vya Syria.

clouds stream