MAREKANI, CUBA KUMALIZA UHASAMA WA MIAKA MINGI ?
Nchi za Marekani na Cuba zimetangaza kukomesha uhasama wa miaka hamsini na kufungua mwanya wa mazungumzo ya kidiplomasia ili kurejesha uhusiano kati yao.
Akitoa tangazo hilo la kihistoria Rais Barrack Obama, amesema kuwa mfumo wa Marekani wa kuitenga Cuba, umeshindwa.
Rais wa Cuba Raúl Castro, ameiomba Marekani kuvunjilia mbali vikwazo vya miaka mitano vya kiuchumi dhidi ya Nchi yake, ambayo anasema vimeiletea nchi hiyo madhara makubwa.
Kuondolewa kwa vikwazo hivyo vitahitaji kupitishwa na Bunge la Congress la Marekani, ambalo linaongozwa na wanachama wengi wa chama pinzani cha Republican. Wengi wao wanapinga ulegezaji kamba kwa vikwazo.