Sunday 21 December 2014

RAIS KIKWETE KUAMUA SAKATA LA ESCROW LEO ?

RAIS KIKWETE KUAMUA SAKATA LA ESCROW LEO ?



Rais Jakaya Kikwete leo anatarajia kulihutubia Taifa  ambapo anatarajiwa kuyatolea ufafanuzi masuala nyeti yanayoligusa taifa hilo ikiwemo sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
Aidha, Rais Kikwete  huenda atatumia siku ya leo kutaja hatua atakazozichukua dhidi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow itakuwa ni moja kati ya agenda muhimu atakayoitolea ufafanuzi.
Hotuba hiyo inakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka vyama mbalimbali vya upinzani pamoja na nchi wahisani   wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kutekeleza azimio la bunge ambalo linatataka mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na sakata hilo la ufisadi wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Miongoni mwa maazimio ya bunge, yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hiyo na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.
Watendaji  wa serikalini wanaodaiwa kuhusika kwa kutowajibika suala lililopelekea upotevu wa mabilioni ya fedha ambazo ni za umma ni Mwanasheria mkuu wa serikali,Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Waziri ardhi, nyumba na maendeleo ya Makazi.
Akaunti ya Escrow ilianzishwa katika Benki Kuu ya Tanzania ili kuhifadhi fedha, baada ya kuibuka kwa mvutano kati ya Shirika la Umeme la Tanzania, Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL kuhusu ongezeko la mtaji wa uwekezaji, huku TANESCO ikilalamika kuwa gharama za kununua umeme kutoka kampuni ya IPTL zilizokuwa kubwa. Fedha hizo zingeendelea kutunzwa katika Akaunti hiyo hadi wakati ambapo suluhisho la mvutano wa wabia hao lingepatikana.

clouds stream