Thursday, 18 December 2014

RAIS KIKWETE KUMALIZA SAKATA LA ESCROW LEO ?

RAIS KIKWETE KUMALIZA SAKATA LA ESCROW LEO ?


Rais Jakaya Kikwete.Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete leo atalihutubia taifa la Tanzania ambapo anatarajiwa kuyatolea ufafanuzi masuala nyeti  ikiwemo  sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo  kisiasa na kijamii wanasema kuwa  huenda  Rais Kikwete atatumia hotuba hiyo kutangaza hatua  atakazozichukua dhidi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow.
Hotuba hiyo inakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya raia na wapinzani wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kutekeleza azimio la bunge ambalo linatataka mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na sakata hilo la ufisadi wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Sakata la Akaunti ya Escrow liliibuliwa bungeni na mmoja wa wabunge wa bunge la Tanzania, David Kafulila na kusababisha mjadala mkali na kuamua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kupewa jukumu la kuchunguza kashfa hiyo.
Kamati hiyo ilikuja na maazimio manane kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na miamala iliyofanyika katika akaunti ya Escrow ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL.
Miongoni mwa maazimio ya bunge yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hiyo na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.

clouds stream