Thursday, 18 December 2014

FIFA ‘YAAMURU’ SIMBA ILIPWE DOLA 300,000 ZA OKWI

FIFA ‘YAAMURU’ SIMBA ILIPWE DOLA 300,000 ZA OKWI



Shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA, limeiamuru klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia kuilipa Simba SC , Dola za kimarekani 300,000 kufuatia ushindi wa kesi ya madai dhidi ya Mshambuliaji Emanuel Okwi.
Simba waliishitaki klabu hiyo kunako Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) baada ya Watunisia hao kukataa kuwalipa Simba pesa za uhamisho wa mchezaji Emanuel Okwi, alipouzwa kutoka Simba kwenda Etoile Du Sahel.
FIFA imeamuru Etoile kuwalipa Simba kiasi hicho ambacho ni zaidi ya Tsh. Milioni 500 za Kitanzania ikiwa ni pamoja na fidia, Awali waligoma wakisema kuwa walikumbwa na ukata wa fedha baada ya kuanza migogoro na Mchezaji huyo pale walipo taka kumkata mshahara alipochelewa kurudi kambini akitokea Uganda alipokwenda kuchezea timu ya Taifa.
Wakati kesi hiyo ikiendeshwa FIFA, ilitoa ruhusa Okwi atafute timu ya kuchezea ili asipoteze kiwango chake, ambapo alirudi Uganda kucheza katika klabu yake ya zamani SC Villa lakini hakuchukua muda akauzwa Yanga SC ya Jijini Dar es salaam, hata hivyo hakukaa sana aliamua kutimkia kunako klabu yake ya Simba na kupewa mkataba wa miezi 6.
Kwa sasa Okwi yupo kwenye mkataba mpya na Simba baada ya jana kusaini mkataba wa miaka 2 kuwatumikia mabigwa hao  wa zamani wa VPL.

clouds stream