SAKATA LA ESCROW LATUA KWA RAIS KIKWETE
Rais Jakaya Kikwete amepokea rasmi ripoti pamoja na ushauri wa Bunge kuhusiana na sakata zima la akaunti ya Tegeta Escrow. Hatua hiyo inafuatia kuanza kazi rami siku ya jumatatu desemba 8, 2014 baada ya kuimarika afya yake kufuatia upasuaji wa tezi dume mwezi mmoja uliopita nchini Marekani.
Kwa mujibu wa kurugezi ya mawasiliano ikulu imesema kwamba Rais kikwete amelekeza kuwa ripoti ya CAG iwekwe hadharani ili kila mwananchi ajue kilichosemwa na kupendekezwa na mdhibiti wa mkuu wa Hesabu za serikali.
Amesisitiza kuwa ripoti hiyo itangazwe kwenye magazeti yanayosomwa na watu wengi pamoja na mitandao ya kijamii ili kila mtanzania aweze kuisoma na kuielewa.
Kwa upande mwingine kufutia kupokea ripoti hiyo rais kikwete anatarajia kuitolea maamuzi baada ya wiki moja kuanzia wiki hii.