Thursday 18 December 2014

97.23% WAFAULU KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA TANZANIA

97.23% WAFAULU KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA TANZANIA


Matokeo ya wanafunzi wa Darasa la saba kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015 nchini Tanzania yametoka huku ongezeko la ufaulu likiwa juu baada ya watoto 438, 960 kati ya 451,392 kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Matokeo hayo yametangazwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Mh. Kassim Majaliwa, mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa osifi za TAMISEMI, jijini Dar es salaam.
Mh. Majaliwa, amesema kuwa, Idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.23 ya wanafunzi waliofaulu mtihani, kwa matokeo hayo yanaonesha kuwa, alama ya juu kabisa kwa wavulana ilikuwa 243 na kwa wasichana 240 kati ya alama 250.
“Waliofaulu mtihani wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule za serikali kwa awamu ya kwanza” Amesema Mh. Majaliwa.
Kwa upande mwingine Mh. Majaliwa, amewaagiza wazazi, walezi, wadau wa elimu na halmashauri zote kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza hapo mapema mwakani.

clouds stream