Breaking News… Bunge Afrika Mashariki lamvua spika madaraka yake
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki kabla ya kubwagwa leo Bi.Margaret Nantongo Zziwa.
Na Mahmoud Ahmad Arusha
BUNGE
la nchi za jumuia ya Afrika Mashariki,lenye makao yake mjini Arusha,
limemvua madaraka ya Uspika wa bunge hilo Margaret Nantongo Zziwa,
kutoka nchini Uganda.
Uamuzi
huo umefanywa leo katika kikao cha bunge hilo ambapo Spika huyo
alipigiwa kura 36 za kutokuwa na Imani nae, kura 2 zimeharika kura moja
haikueleweka hivyo kukosa sifa ya kuendelea na wadhifa huo.
Kwa
mujibu wa kanuni ya 32 ya bunge la jumuia hiyo ya Afrika Mashariki
inatakiwa theluthi mbili ya wabunge sawa na kura 30 kumung’oa Spika.
Sababu
za kuondolewa madarakani ni kushindwa kutimiza majukumu kama Spika,
matumizi mabaya ya kiti hicho kwa kuwapendelea ndugu ambao wameajiriwa
ndani ya bunge hilo .
Sababu
nyingine anadaiwa kuwa na kauli mbaya dhidi ya wabunge na wafanyakazi
wa bunge hilo, mume wake kuingilia shughuli za utendaji wa bunge kinyume
na taratibu.
Mwenyekiti
wa kamati ya uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili Spika wa
EALA, Mh. Frederic Ngenzebuhoro akisoma ripoti ya kamati yake
iliyopelekea spika huyo kuong’olewa.
Wametoa
saa 48 kwa wabunge wa Uganda,kujaza fomu kwa ajili ya kuomba nafasi
hiyo ya Spika, kwa kuwa bado ni zamu ya Uganda kukalia kiti hicho.
Maazimio
hayo yamesomwa na Frederic Ngenzebuhoro, ambae ni mbunge wabunge hilo,
pia ni mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Spika huyo.
Ngezabuhilo,amesema
tuhuma zote dhidi ya Spika huyo zimethibitika hivyo wabunge kwa kauli
moja wameamua kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika huyo .
Wakati
wa maamuzi hayo spika hakuwepo bungeni huku mwanasheria wake, Gety
Tumwebaze ,kutoka Uganda,amesema spika anapinga kikao hicho, ni batili
na maamuzi yatakayotolewa hawatayakubali kwa kuwa yapo nje ya taratibu
za bunge hilo.
Mheshimiwa Hafsa Moss akichangia mjadala wa kamati uliopewa kuchunguza tuhuma mbalimbali zinazomkabili spika huyo.
Mh. Mukasa Mbidde akishiriki zoezi la upigaji kura lililopelekea kung’olewa kwa spika huyo.