Sakata la Gwajima: Polisi Wamhoji Kwa Masaa Matano..... Atakiwa
Kurudi Polisi Wiki Ijayo na Hati ya Usajili wa Kanisa
Lake,Helkopta na Viwanja Anavyomiliki
Askofu
wa Kanisa la Ufufua na Uzima Josephat Gwajima amelitikisa tena Jiji
la Dar es Salaam jana mara baada kuwasili makao makuu ya Jeshi la
polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ili kuendela na mahojiano
kuhusu tuhuma za kumkashfu Askofu Pengo.
Gwajima
aliwasili Makao Makuu ya Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
Majira ya saa mbili kamili asubuhi huku akisindikizwa na viongozi mbali
mbali wa Kanisa la Ufufuo na Uzama pamoja na Mwanasheria wake .
Eneo
lote la kituo hicho cha polisi lilikuwa chini ya ulinzi mkali
wa maofisa mbalimbali wa Usalama wa Taifa wakisaidiwa na Jeshi la
Polisi.
Baada
ya kuwasili kituoni hapo, umati mkubwa wa Waumini wake ulizunguka
maeneo yote ya Kituo hicho huku wengine wakiwa maeneo ya stendi ya
Treni ya Reli ya kati.
Kama
kawaida, Waumini hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali ambazo
wanadai zilikuwa mahususi kumpa nguvu Askofu huyo ajibu kesi hiyo kwa
ufasaha.
Baada
ya Mahojiano ya takribani masaa Matano, hatimaye Askofu Gwajima
alitoka ndani ya kituo hicho,lakini katika hali isiyo ya
kawaida,Askofu huyo aligoma kuongea na vyombo vya habari.
Baada ya Gwajima kugoma kuongea,mwandishi wetu alimfuata Mwanasheria wake aliyekuwa ameambatana naye,John Mallya ambaye alisema kuwa mteja wake alikuwa amechoka, hivyo asingeweza kuongea.
Mallya alimweleza mwandishi kuwa mambo aliyohojiwa Gwajima ni kuhusu mali zake na sio matamshi ya kumtukana Askofu Pengo.
“Mahojiano
yamekwenda vizuri lakini nasikitika sana kutokana na mambo waliyokuwa
wanamhoji. Wamemuuliza mambo ambayo hayahusiani kabisa na kile
tulichotarajia na ndicho kilichotuleta hapa, nilidhani mteja wangu
ataulizwa kuhusiana na matumizi ya lugha chafu iliyodaiwa kutumika
kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini,” alihoji wakili wa Gwajima.
Aliendelea
kusema kuwa, mambo aliyoulizwa ni kuhusiana na ukoo wake, wazazi wake
hata ndugu zake na watu wengine wa kwao waliokufa.
Alisema
walihoji pia juu ya mambo mengine kama umiliki wa helikopta, utajiri
wake, nyumba anayoishi, uhusiano wake na watu mbalimbali.
“Nimeshangaa
sana kuona mteja wangu ameulizwa vitu kama hivyo ambavyo havihusiani na
madai ya hapo awali ya matumizi ya lugha ya matusi. Tumeagizwa tulete
nyaraka kumi siku ya mahojiano yetu tena yatakayofanyika tarehe 16 mwezi
huu na sisi tutafanya hivyo,” alisema Mallya.
Alizitaja
nyaraka na vitu vingine wanavyotakiwa kuvipeleka Aprili 16 ni hati ya
usajili wa kanisa, bodi ya udhamini wa kanisa na majina yao, idadi ya
makanisa yaliyopo chini yake, na muundo wa uongozi wa kanisa lake.
Vingine
ni namba ya usajili wa kanisa, ritani za kanisa lake (mapato na
matumizi ya fedha za kanisa lake), mtu anayechukua na kurekodi mkanda wa
video kanisani kwake, pamoja na waraka wa Baraza la Maaskofu uliosomwa
makanisani.