Tuesday, 26 May 2015
Real Madrid wafukuza kocha
Real Madrid wafukuza kocha
Tarehe May 26, 2015
Baada ya kushindwa kuifikisha Real Madrid kwenye hatua ya fainali kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya na pia kushindwa kuchukua ligi kuu nchini Hispania imekuwa kama moja ya mambo yaliyofanya kocha wa Carlo Ancelotti kufukuzwa. Carlo Ancelotti alipofanya mahojiano na waandishi wa habari siku ya ijumaa alisema anaamini ataendelea kuifundisha timu hiyo msimu ujao huku wachezaji kama Cristiano Ronaldo na James Rodriguez wakiamini kuwa na kocha wao msimu ujao.
Maamuzi ya Real Madrid kumfukuza Carlo Ancelotti yalifanyika jana baada ya rais wa timu hiyo Florentino Perez kuonyesha wazi siku za karibuni kwa maneno yake kuwa kocha huyo amebakiza siku chache kwenye klau hiyo, nuamuzi huo wa Real Madrid unaongeza tetesi kwenye masikio ya mashabiki wa Real Madrid kuwa kocha atakaechukua kiti hicho ni Rafa Benitez.
Baada ya kushindwa kuifikisha Real Madrid kwenye hatua ya fainali kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya na pia kushindwa kuchukua ligi kuu nchini Hispania imekuwa kama moja ya mambo yaliyofanya kocha wa Carlo Ancelotti kufukuzwa. Carlo Ancelotti alipofanya mahojiano na waandishi wa habari siku ya ijumaa alisema anaamini ataendelea kuifundisha timu hiyo msimu ujao huku wachezaji kama Cristiano Ronaldo na James Rodriguez wakiamini kuwa na kocha wao msimu ujao.
Maamuzi ya Real Madrid kumfukuza Carlo Ancelotti yalifanyika jana baada ya rais wa timu hiyo Florentino Perez kuonyesha wazi siku za karibuni kwa maneno yake kuwa kocha huyo amebakiza siku chache kwenye klau hiyo, nuamuzi huo wa Real Madrid unaongeza tetesi kwenye masikio ya mashabiki wa Real Madrid kuwa kocha atakaechukua kiti hicho ni Rafa Benitez.
Dkt.Kikwete amteua mkuu mpya wa Wilaya na kuwahamisha wengine 10
Dkt.Kikwete amteua mkuu mpya wa Wilaya na kuwahamisha wengine 10
Rais Jakaya Kikwete amemteua Bw. Antony Peter mavunde kuwa mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imebainisha kwamba licha ya kumteua mkuu wa wilaya mpya mmoja pia awahamisha wakuu wa wilaya wengine 10 kwa lengo la kuongeza ufanisi katika wilaya mbalimbali nchini.
Katika mabadiliko hayo,Rais kikwete amemhamisha Luteni Edward ole Lenga kutoka wilaya ya Mkalama mkoni Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni kanali benedict Kulikela kitenga ambaye alifariki dunia aprili 20 mwaka huu.
Wengine ni Elizabeth Chalamila Mkwasa kutoka wilaya ya Dodoma kwenda wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro. Dkt Jasmine Tisike kutoka wilaya ya Mpwapwa kwenda Dodoma. Agnes Elias Hokololo kutoka wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwenda wilaya ya Tunduru, Fadhili Nkurlu kutoka wilaya ya Misenyi mkoani kagera kwenda wilaya ya mkalama.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Chande Bakari Nalicho amehamishwa kutoka wilaya ya Tunduru kwenda Wilaya ya Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka wilaya ya Mvomero kwenda Misenyi , Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Karagwe mkoani Kagera kwenda wilaya ya biharamulo mkoani humo humo.
Elias Choro John Tarimo amehamishwa kutoka wilaya ya Biharamulo kwenda wilaya ya Chunya mkoani mbeya pamoja na Deodatus Lukasi Kinwiro kutoka wilaya ya Chunya kwenda wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Burkina Faso: Madaktari kupima DNA Mwili wa aliyekuwa Rais Thomas Sankara
Burkina Faso: Madaktari kupima DNA Mwili wa aliyekuwa Rais Thomas Sankara
Tarehe May 26, 2015
Ripoti za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unaokisiwa kuwa wa raisi wa zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka kubainisha ikiwa ni wake.
Familia na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku ya kutaka kufahamu iwapo mabaki hayo ni yake.
Bwana Sankara aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987. Sankara alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983.
Sankara alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika mji mkuu wa wa nchi hiyo Ouagadougou
Madaktari wawili kutoka Burkina Faso na mmoja kutoka Ufaransa watachukua chembechembe za mwili huo na kuipima wakitumia mashine na mbinu za kisasa za DNA ilikubaini kikamilifu iwapo inahusiana na mwili wa Sankara.
Miili mingine 12 ya wafuasi wake waliouawa pamoja naye pia itafukuliwa.
Mabaki hayo ya Sankara yamezikwa katika makaburi ya Dagnoen katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Ripoti za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unaokisiwa kuwa wa raisi wa zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka kubainisha ikiwa ni wake.
Familia na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku ya kutaka kufahamu iwapo mabaki hayo ni yake.
Bwana Sankara aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987. Sankara alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983.
Sankara alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika mji mkuu wa wa nchi hiyo Ouagadougou
Madaktari wawili kutoka Burkina Faso na mmoja kutoka Ufaransa watachukua chembechembe za mwili huo na kuipima wakitumia mashine na mbinu za kisasa za DNA ilikubaini kikamilifu iwapo inahusiana na mwili wa Sankara.
Miili mingine 12 ya wafuasi wake waliouawa pamoja naye pia itafukuliwa.
Mabaki hayo ya Sankara yamezikwa katika makaburi ya Dagnoen katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Mafuriko yaikumba Texas, watu 18 wafariki dunia
Mafuriko yaikumba Texas, watu 18 wafariki dunia
Mafuriko yamesababisha vifo vya watu 18 Magharibi mwa Marekani na Kaskazini mwa Mexico.
Wengi wa waliothibitishwa kufariki dunia kutokana na mafuriko hayo ni kutoka mpakani mwa Mexco katika mji wa Acuna.
Hata hivyo katika mji wa Texas watu watatu wamearifiwa kufa pia na wengine 12 hawajulikani waliko baada ya makazi yao kusombwa na mafuriko.
Gavana wa Texas Greg Abbott anasema mafuriko hayo yameleta madhara makubwa katika jimbo lake.
NEC yatoa ratiba Uchaguzi mkuu 2015
NEC yatoa ratiba Uchaguzi mkuu 2015
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa rasmi ratiba kwa vyama vya Siasa na wananchi wote itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika Agosti 21, 2015, na kampeni za Uchaguzi kwa wagombea hao zitatarajia kuanza Agosti 22 mpaka – Oktoba 24 mwaka huu.
Siku ya kupiga kura kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015 kwa wale waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
Ufisadi watikisa Kenya, Mawaziri 4 matatani
Ufisadi watikisa Kenya, Mawaziri 4 matatani
Mkuu wa mashtaka ya umma nchini Kenya Keriako Tobiko, hii leo amebainisha yaliyomo katika hati za kesi za mawaziri wanne wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
Tume ya maadili na kupambana na ufisadi ya Kenya imependekeza kuwa waziri wa uchukuzi Mhandisi Michael Kamau na waziri wa leba Kazungu Kambi kushtakiwa na matumizi mabaya ya ofisi.
Mhandisi Michael Kamau anakumbwa na shutuma za kutumia fedha ubadhirifu wa fedha za umma na kufanya mabadiliko katika ubunifu wa barabara ambayo tiyari ilikuwa imetengenezwa na mashauri.
Kazungu Kambi naye anadaiwa keteuwa wanachama wawili katika bodi ya shirika la taifa la hazina ya uzeeni kinyume na sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari afisa mkuu wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi Halakhe Waqo, alisema kwamba mawaziri wanne waliochunguzwa ni waziri wa Uchukuzi Mhandisi Michael Kamau, waziri wa ardhi, makao na ustawi wa miji bi Charity Ngilu, waziri wa kilimo Felix Kosgei, waziri wa leba Kazungu kambi, seneta wa Nairobi Mike Sonko na mbunge .
Tume hio imemwandikia rais Uhuru Kenyatta ombi la kuongeza muda wa uchunguzi wa kesi zilizobaki. Siku sitini ambazo walikuwa wamepewa kukamilisha uchunguzi wa ripoti hiyo zimetimia leo.
Kwa sasa tume hio imekamilisha kesi 56 kati ya 124 zilizowasilishwa kwa uchunguzi zaidi baada ya ripoti yao ya awali iliyokabidhiwa rais Kenyatta kuwasilishwa bungeni . Kesi 21 tayari zimefikishwa kwa mkuu wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko.
Kufikia sasa maafisa 19 wamefikishwa mahakamani na wengine 29, kulingana na afisa mkuu wa EACC, watafikishwa mahakamani siku chache zijazo katika maeneo kadhaa nchini yakiwemo Turkana, Machakos, Nyamira, Nairobi na Trans nzoia.
Burundi: Maandamano yapamba moto, basi lachomwa moto
Burundi: Maandamano yapamba moto, basi lachomwa moto
Basi moja la uchukuzi limechomwa moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wamechoma moto magurudumu katika eneo la Kanyosha. Kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano hayo dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.
Maandamano haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.
Aidha wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutatua mzozo ulioko wa kisiasa.
Uamuzi ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki kadhaa.
Hadi sasa tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa jirani ikiwemo nchini Tanzania.
Lowassa alipua upya sakata la Richmond, alia na Mwakyembe
Lowassa alipua upya sakata la Richmond, alia na Mwakyembe
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa ameibuka kwa mara ya kwanza na kuzungumzia sakata la Richmond lililopelekea kujiuzulu cheo cha Uwaziri mkuu febriari 7 mwaka 2008.
Akizungumza na Wahariri leo nyumbani kwake mkoani Dodoma Edward Lowassa amesema kwamba hausiki kabisa na sakata ka Richmond na ndio sababu hata kamati a Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji.
Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari akiwa ameambatana na Nazir Kalamagi, Peter Selukamba, Diana Chilolo, Hussein Bashe ikiwa ni baadhi ya walio athirika kutokana na sakata la Richmond. Katika mkutano huo pia amemtangaza Elizabeth Msoki kuwa mkurugenzi wa mahusiano na Mawasiliano katika timu yake ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Ameongeza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio lilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na Spika wa Bunge wa wakati huo ambaye alikuwa ni Samweli Sitta. Hicho sio kikwaz kwake katika safari yake ya kuingia ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua huku akiahidi kuchukua muda mrefu zaidi kulizungumzia sakata hili hususani mwishoni mwa wiki hii mkoani Arusha.
Lowassa alijiuzulu februari 7 mwaka 2008 kutokana na madai ya kuhusika ktika kashfa ya kuibeba kampuni ya Richmond Development (LLC) ya nchini Marekani katika mchakato wa upatikanaji wa zabuni ya umeme wa dharura hapa nchini.
Akizungumzia malengo yake Lowassa amesema serikali ya Jakaya ilikosea kuanza kilimo na kuweka kando elimu huku akisisitiza sera yake itakuwa ni elimu kwanza.
Kwa upande wa Pesa za kampeni amesema anapata kutokana na michango ya rafiki zake na ataendelea na kupata michango hiyo.
Alipoulizwa kuhusu mpango wa kuhama Chama chake endapo atatatoswa na kamati kuu (CCM) amesema asiyempenda ndani ya chama hicho atahama yeye kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi ya kuwania Urais huku akisisitiza kuwa hatalipa kisasi kwa jambo lolote lililomtokea katika safari yake ya kisiasa ikiwemo sakata la Richmond.
Hata hivyo amesema Arusha itwaka moto tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania kutega sikio kwani ata aanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi hii na mipango yake ya kuinua nchi kuichumi katika miaka kumi ijayo.
CCM yatoa ratiba uchukuaji fomu za Urais
CCM yatoa ratiba uchukuaji fomu za Urais
Tarehe May 25, 2015
Kikao cha halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (NEC) imetoa ratiba ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi huku nafasi ya urais wa jamuhuri ya muungano wagombea wakitakiwa kuchukua fomu kuanzia June tatu mpaka Julai mbili mwaka huu.
Akizungumzia ratiba hiyo katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye amesema wagombea urais wa jamuhuri ya muungano na ule wa Zanzibar watatakiwa kuchukua fomu kuanzia tarehe tatu june na kuzirudisha tarehe 2 julai.
Katika kipindi hicho pamoja na mambo mengine watatakiwa kutafuta wadhamini wasipopungua 450 kwa nafasi ya jamuhuri kutoka Mikoa 15 mitatu kati yake iwe Zanzibar na urais wa Zanzibar wadhamini 250 kutoka mikoa mitatu ya Zanzibar.
Mara baada ya zoezi hilo litafuatiwa na vikao mbalimbali vya uchujaji wa majina ya wagombea kwa kuanza na kikao cha kamati ya usalama na maadili tarehe 8/7 kikifuatiwa na kikao cha kamati kuu tarehe 9/7 halafu halmashauri kuu ya CCM NEC itakayotoa jina la mgombea wa urais tarehe 10/7 na kisha mkutano mkuu utakaofanyika tarehe 12/13 mwezi jully.
Kwa upande wa nafasi za ubunge na udiwani na baraza la wawakilishi wagombea watatakiwa kuchukua fomu kuanzia tarehe 15-19 mwezi jully ambapo kampeni za ushawishi kwa wanachama kwenye matawi zitafanyika kuanzia tarehe 20 mpaka 31 jully.
Kura za maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea katika ngazi hizo zitapigwa sambamaba tarehe 1/08 2015 huku wagombea wote wakitakiwa kuzingatia maelekezo ya kanuni na taratibu za chama hicho.
Kikao cha halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (NEC) imetoa ratiba ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi huku nafasi ya urais wa jamuhuri ya muungano wagombea wakitakiwa kuchukua fomu kuanzia June tatu mpaka Julai mbili mwaka huu.
Akizungumzia ratiba hiyo katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye amesema wagombea urais wa jamuhuri ya muungano na ule wa Zanzibar watatakiwa kuchukua fomu kuanzia tarehe tatu june na kuzirudisha tarehe 2 julai.
Katika kipindi hicho pamoja na mambo mengine watatakiwa kutafuta wadhamini wasipopungua 450 kwa nafasi ya jamuhuri kutoka Mikoa 15 mitatu kati yake iwe Zanzibar na urais wa Zanzibar wadhamini 250 kutoka mikoa mitatu ya Zanzibar.
Mara baada ya zoezi hilo litafuatiwa na vikao mbalimbali vya uchujaji wa majina ya wagombea kwa kuanza na kikao cha kamati ya usalama na maadili tarehe 8/7 kikifuatiwa na kikao cha kamati kuu tarehe 9/7 halafu halmashauri kuu ya CCM NEC itakayotoa jina la mgombea wa urais tarehe 10/7 na kisha mkutano mkuu utakaofanyika tarehe 12/13 mwezi jully.
Kwa upande wa nafasi za ubunge na udiwani na baraza la wawakilishi wagombea watatakiwa kuchukua fomu kuanzia tarehe 15-19 mwezi jully ambapo kampeni za ushawishi kwa wanachama kwenye matawi zitafanyika kuanzia tarehe 20 mpaka 31 jully.
Kura za maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea katika ngazi hizo zitapigwa sambamaba tarehe 1/08 2015 huku wagombea wote wakitakiwa kuzingatia maelekezo ya kanuni na taratibu za chama hicho.
Friday, 22 May 2015
Taifa Stars nje michuano ya COSAFA
Taifa Stars nje michuano ya COSAFA
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) jana imepoteza mchezo wa pili mfululizo katika michuano ya kombe la Cosafa, baada ya kufungwa mabao 2 – 0 na Madagascar, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.
Kwa Taifa Stars kupoteza mchezo huo, moja kwa moja inakua imeaga michuano katika hatua ya makundi, kutokana na kubakisha mchezo mmoja tu wa kukamilisha ratiba dhidi ya Lesotho utakaochezwa kesho ijumaa katika uwanja wa Moruleng.
Katika mchezo huo wa jana, Taifa Stars ilishindwa kuonyesha makali yake mbele ya timu ya Madagascar na kupelekea kufungwa mabao 2 katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Sehemu ya ushambuliaji ya Taifa Stars haikua na madhara yoyote langoni mwa Madagascar, huku sehemu ya ulinzi iLijikuta na wakati mgumu muda wote kuzuia hatara za washambuliaji wa Madagascar.
Mara baada ya mchezo huo, kocha wa Stars Mart Noij alisema amesikitishwa na matokeo hayo, kwamba hakutegemea kupoteza mchezo dhidi ya Madagascar.
“Timu yangu haikucheza vizuri, haikuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga , huku wapinzani awetu wakitumia nafasi mbili walizozipata kupata mabao mawili katia mchezo huo” alisema Nooij.
Mpaka sasa kundi B la linaongozwa na Madagscar yenye ponti 6 sawa na Swaziland yenye pointi 6 pia zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, na mchezo wa mwisho utakaowakutanisha kesho ndio utakaoamua nani atatinga hatua ya robo fainali.
Kufuatia Taifa Stars kupoteza michezo yote miwili, inaungana na Lesotho kutoka kundi B kuaga michuano hiyo, huku kundi A timu za Mauritius na Shelisheli zikiwa zimeshaaga michuano hiyo pia.
Stars inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kesho iumaa usiku mara baada ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho utakochezwa kesho jioni.
Urais 2015: Mwanamke wa kwanza CCM ajitokeza kutangaza nia
Urais 2015: Mwanamke wa kwanza CCM ajitokeza kutangaza nia
Mwanamke wa Kwanza ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) Amina Salum Ali, amevunja ukimya na kuamua kuweka wazi nia yake ya kutaka kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba.
Akizungumzia uamuzi huo, mwanasiasa huyo ambaye pia ni Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) katika Umoja wa Mataifa (UN), amesema wanawake wamekuwa wanyonge kugombea nafasi za juu za uongozi kwa kukosa fedha, lakini sasa ni wakati mwafaka kwao kujiamini katika jamii kwani uongozi siyo fedha bali ni uzalendo, kujikubali na kujiamini.
“Nimeona nina uzalendo, ninajiamini na ninaweza kuifikisha nchi yangu katika uchumi wa kwanza kwa kutumia rasilimali zetu zikiwamo gesi, mafuta, kilimo na utalii. Ninajiamini kwamba wakati wangu umefika kuwaongoza Watanzania.” amesema Amina
Amina ambaye aliwahi kushika nafasi za juu za uongozi Zanzibar na Tanzania Bara, ukiwamo uwaziri wa fedha Zanzibar.
Ameongeza kuwa wanawake wengi wanaogopa kujitokeza wakihofia kugombea nafasi za juu za uongozi kwamba kunahitaji fedha hivyo wanaishia kuwa wanyonge. Siyo kweli, wajitokeze kwa wingi ili kitimiza ndoto za kuwajibika kwa taifa letu,” alisema.
Amina anaungana makada wengine wanaotajwa kuwania Urais mwaka huu ambao ni mawaziri wakuu wastaafu, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja , Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi , Teknolojia, January Makamba pamoja na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangalah.
Mtu mmoja auawa kwenye Maandamano Burundi
Mtu mmoja auawa kwenye Maandamano Burundi
Mtu huyo alikuwa miongoni mwa waandamanaji wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa awamu ya tatu.
Walioshuhudia wanasema kuwa polisi walimpiga mwandamanaji huyo risasi mgongoni wakiwa katika eneo la Musaga linalotazamwa kama ngome ya upinzani.
Waandamanaji walijaribu kufika katikati mwa jiji la Bujumbura lakini walitimuliwa kwa mabomu ya moshi wa kutoa machozi.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewaomba zaidi ya raia laki moja na hamsini waliokimbia ghasia nchini humo katika majuma kadhaa yaliyopita, warejee nyumbani.
Marekani yaomba radhi vifo vya watoto Syria
Marekani yaomba radhi vifo vya watoto Syria
Marekani imekiri, kwa mara ya kwanza kuhusika na mapigano ya anga dhidi ya kikosi cha kiislamu yaliyopelekea baadhi ya raia kuuawa. Katika mkutano wa dharula Pentagon Mkuu wa kikosi Luteni Jenerali James Terry ,aliomba radhi kwa mauaji ambayo yalitokea bila kukusudia na kuua watoto wawili waliouawa wakati wa machafuko nchini Syria mwaka jana.
Kufuatia tukio lililotokea mjini Palmyra na Ramadi katika kipindi cha wiki limehusishwa kama kisasi . Ingawa Rais Obama alisisitiza kuwa Marekani ilikuwa si ya kupoteza vita na wapiganaji . Rais aliahidi msaada zaidi kwa vikosi vya usalama nchini Iraq na kusema Marekani itajaribu kuongeza mafunzo ya kijeshi katika maeneo ya Sunni.
Siku moja baada ya mji wa Syria wa Palmyra kuanguka , Wakazi wa eneo hilo wanasema waislamu wenye siasa kali bado wanawasaka wale wanaounga mkono serikali.
Hata hivyo wapiganaji wa Kiislamu wameripotiwa kuwa wengi zaidi ya ulinzi wa eneo la mashariki mwa Iraq, huku wakijaribu himaya yao huko.
Monday, 18 May 2015
BREAKING: Simba wamuacha rasmi kocha wake
Barcelona bingwa La Liga
Barcelona bingwa La Liga
Lionel Messi amewapa Barcelona ubingwa wa La Liga msimu wa 2014-2015 baada ya kuifungia timu yake bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Atletico Madrid kwenye uwanja wa Vicente Calderon.
Messi amefunga goli hilo katika dakika ya 65 akimalizia pasi ya Pedro Rodriguez.
Kwa matokeo hayo Barcelona wamefikisha pointi 93 baada ya kushuka dimbani mara 37 na wamebakiza mechi moja.
Real Madrid wameshinda magoli 4-1 kwenye mchezo wa leo dhidi ya Espanyol na kufikisha pointi 89 baada ya mechi 37 walizocheza.
Kwa maana hiyo wakishinda mechi ya mwisho watafikisha pointi 92 ambazo tayari zimeshavukwa na Barcelona.
Inawezekana msimu ukawa mkubwa kwa Barcelona, leo wameshatwaa taji la ligi kuu (La Liga) na watacheza fainali mbili, ligi ya mabingwa barani Ulaya na kombe la mfalme ‘Copa del Rey’.
Mbali na machungu ya timu yake kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya katikati ya wiki hii na leo kukosa ubingwa wa La Liga, mshambuliaji hatari wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amefunga magoli matatu peke yake ‘hat-trick’ katika ushindi wa Madrid wa goli 4-1.
Ronaldo amefunga magoli hayo katika dakika ya 59, 83 na 90. Goli lingine limefungwa na Marcelo dakika ya 79 wakati goli la kufutia machozi kwa Espanyol limefungwa na Cristian Stuani dakika ya 73.
Watu 9 wauawa,18 wajeruhiwa katika shambulio
Watu 9 wauawa,18 wajeruhiwa katika shambulio
Polisi nchini Marekani wamesema kuwa watu tisa wameuawa na watu wengine 18 kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki katika mgahawa mmoja katika mji wa Waco.
Kwa mujibu wa maofisa katika mji huo wanasema kuwa walibaini mkusanyiko kati ya watu watano walioonekana kupanga jambo lisilo la kawaida.
Watu hao waliokuwa katika mgahawa huo walijificha katika chumba cha majokofu katika harakati za kujiokoa kabla ya kusaidiwa na Polisi kutoka katika eneo hilo.
Nkurunziza atoa onyo kwa Al shabaab, Wamarekani watimka Burundi
Nkurunziza atoa onyo kwa Al shabaab, Wamarekani watimka Burundi
Rais Nkurunziza akihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya Bujumbura alionya kuwa kuna tishio la shambulizi la kigaidi kutoka kwa kundi la waislamu kutoka Somalia wenye uhusiano na Al-Qaeda , Al Shabaab.
Aliwaambia wandishi wa habari wa kimataifa kuwa tishio hilo la mashambulizi sio tu kwa taifa lake bali pia kwa Kenya na Uganda .
Hata hivyo, Nkurunziza hakuzungumzia lolote kuhusu hali ilivyo nchini Burundi wala tishio la mapinduzi dhidi yake.
Kwa upande wa Wapinzani wake wanasema huenda hiyo ni njama ya rais Nkurunziza kuidhinisha makabiliano makali dhidi ya wapinzani wake ambao tayari wameagiza wafuasi wao kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuendelea na maandamano ya kumtaka asiwanie kipindi cha tatu katika kura za urais zitakazofanyika mwezi
Tishio la Al Shaabab dhidi ya Burundi li kufuatia mchango wake katika jeshi la umoja wa Afrika Amisom huko Somalia.
Marekani tayari imeagiza raia wake kuondoka nchini humo kufuatia tishio la shambulizi la kigaidi mbali na kuzorota kwa hali ya usalama.
Rais Morsi ahukumiwa kifo
Rais Morsi ahukumiwa kifo
Mahakama nchini Misri imetoa amri ya kunyongwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi.
Mahakama hiyo ilimpata na hatia aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi kufuatia kuvunjwa kwa magereza mwaka wa 2011.
Kauli hii ni msumari katika kidonda cha Morsi ambaye alikuwa tayari anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kuamrisha kukamatwa kwa waandamanaji waliopinga utawala wake.
Morsi aling’olewa mamlakani na jeshi mwezi Julai mwaka wa 2013 kufuatia kipindi kirefu cha maandamano dhidi ya utawala wake.
Kuanzia hapo chama chake cha the Muslim Brotherhood kimepigwa marufuku huku mamia ya maelfu ya wafuasi wake kukamatwa na vyombo vya dola.
Kufuatia uamuzi huo wa kifo , sasa kauli nzima na ruhusa itapatikana tu baada ya uamuzi kutumwa kwa kadhi mkuu nchini humo ambaye sasa ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho iwapo Morsi ataonja mauti au la .
Sheria za nchi hiyo hata hivyo zinamruhusu Morsi kukata rufaa licha ya uamuzi wa kadhi mkuu.
Hata hivyo Rais Morsi amekataa katakata uhalali wa mahakama iliopo sasa. Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru.
Share
Wednesday, 13 May 2015
Azam yatoa ufafanuzi ujio wa Stewart Hall
Azam yatoa ufafanuzi ujio wa Stewart Hall
Baada ya taarifa kuzagaa juu ya uongozi wa Azam FC kumrudisha kocha wa zamani wa kikosi hicho Muingereza Stewart Hall, uongozi wa klabu hiyo umevunja ukimya kwa kuamua kutoa ufafanuzi juu ya tetesi hizo.
Mwenyekiti wa klabu hiyo Said Mohamed amesema, kwa sasa klabu yao ipo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mwingine lakini kwenye orodha ya majina ya makocha wanaotaka kuwapa kibarua cha kukinoa kikosi chao ni pamoja na jina la Stewart Hall.
“Sisi sasa hivi tupo kwenye mchakato wa kutafuta mwalimu, kwahiyo majina yanakuwa mengi sana. Tuna majina karibu 12 mpaka sasa hivi, moja kati ya hayo ni la Stewart, lakini bado hatujakaa kikao cha kuchuja ili kupata jina moja”, amesema Mohamed.
Alipoulizwa kuhusu hatma ya George Nsimbe ‘Best’, Mohamed alisema, “George yeye alipewa kazi ya kuwa ‘care taker coach’ baada ya kuondoshwa Omog, sasa sio lazima apewe majukumu ya ukocha mkuu”, Mohamed alifafanua.
“Tukishapitisha jina tutalipeleka kwenye bodi ya timu, baada ya kila kitu kuwa kimekamilika, tutawaita waandishi wa habari na tutawaambia kila kitu ambacho kimeamuliwa”, alimaliza.
Hall alitimuliwa na uongozi wa Azam katikati ya msimu wa 2012-2013 na nafasi yake ikachukuliwa na kocha raia wa Cameroon Joseph Omog ambaye nae kibarua chake kiliota nyasi baada ya mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu Tanzania bara kutupwa nje ya michuano ya vilabu bingwa Afrika na nafasi yake kuchukuliwa na Nsimbe ambaye alimalizia mechi zilizo salia kwenye ligi kuu huku akifanikiwa kuisaidia Azam kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Yanga ambao ni mabingwa.
Mzozo wa matangazo wazua mgogoro mkubwa La Liga
Mzozo wa matangazo wazua mgogoro mkubwa La Liga
Hakuna maendeleo kwenye mkutano kati ya wakuu wa liga na vilabu nchini mpaka kuzua mshtuko mkubwa kuhusu uwezekano wa kukosekana kwa mechi za mwishoni mwa juma.
Serikali nchini Hispania ilitangaza makualiano mapya juu ya kuweka usawa zaidi kwenye ligi kwa kuondoa uwepo wa makubaliano ya matangazo ya televisheni ya vilabu vyenye nguvu nchini Hispania ambavyo ni Real Madrid na Barcelona.
Makubaliano haya ndio yanasababisha mgomo kwa vilabu unaotarajiwa kuanzia mei 16, mgomo huu utaathiri mechi za fainali za ligi ya mabingwa barani ulaya itakayochezwa juni 6 na na Copa Amerika.
Pluijm aweka hadharani kikosi bora VPL 2014-2015
Pluijm aweka hadharani kikosi bora VPL 2014-2015
Msimu wa 2014-2015 wa ligi kuu ya soka Tanzania bara umemalizika mwishoni mwa juma lililopita (Mei 9 mwaka huu) na kushuhudia Yanga wakitangazwa mabingwa, Azam wakishika nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu, Mbeya City nafasi ya nne, huku Ruvu Shooting na Polisi Morogoro zikishuka daraja.
Kila kocha anapewa nafasi ya kutaja kikosi cha wachezaji 11 kutoka timu zote zilizoshiriki ligi kuu msimu uliopita ambao anaona wanaingia katika kikosi chake bora kwa msimu uliomalizika hivi karibuni.
Leo tunaanza na kocha aliyetwaa ubingwa akiifundisha Yanga, Hans van der Pluijm ambaye amewataja wachezaji 11 anaoona wameonesha ubora wa hali ya juu kwenye msimu huu.
“Golini namuweka Ally Mustafa, nadhani amecheza vizuri sana, beki wa kulia ni Juma Abdul, mabeki wa katikati nawaweka Paschal Wawa na Nadir Haroub, kushoto Tshabalala kutoka Simba, sijui jina lake, najua jina lake la utani ni Tshabalala”, amesema Pluijm.
“Safu ya kiungo ni Said Ndemla kutoka Simba, winga wa kulia ni Msuva, winga wa kushoto Emmanuel Okwi, kiungo wa mbele Niyonzima na washambuliaji wawili ni Amissi Tambwe na Kavumbagu”, Pluijm alimaliza kikosi chake.
“Sikuwepo wakati ligi inaanza, nilianza kazi Yanga mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, lakini kwa kipindi nilichoona ligi nimewaona wachezaji hao kuwa bora zaidi msimu huu”, Pluijm alimaliza.
Kwa mujibu wa van der Pluijm, kikosi bora cha msimu uliomalizika wa 2014-2015 kinaundwa na wachezaji wafuatao, kwenye mabano ni timu wanazotokea.
- Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga SC)
- Juma Abdul (Yanga SC)
- Mohamed Hussein ‘Tshabala’ (Simba SC)
- Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC)
- Paschal Wawa (Azam FC)
- Said Ndemla (Simba SC)
- Simon Msuva (Yanga SC)
- Haruna Niyonzima (Yanga SC)
- Amis Tambwe (Yanga SC)
- Didier Kavumbagu (Azam FC)
- Emmanuel Okwi (Simba SC)
Kufa au kupona leo: Real vs Juventus
Kufa au kupona leo: Real vs Juventus
Juventus inaelekea kwenye mchezo wa raundi ya pili ligi ya mabingwa barani ulaya ikiwa na hazina ya magoli 2 iliyoyapata kwenye ushindi wa magoli 2-1 mjini Turin kwa magoli ya Álvaro Morata na Carlos Tévez. Timu zote mbili zilikutana msimu uliopita kwenye makundi baada Madrid kupata ushindi wa 2-1 nyumani kabla ya kutoka sare ya 2-2 jijini Turin.
Real Madrid ameshinda mara 21 katika michezo 29 dhidi ya timu za Italia na kutoka sare mara mbili na pia rekodi nzuri ya kucheza michezo 11 bila kufungwa kabla ya kupoteza kwa 4-3 dhidi ya FC Schalke 04 licha ya Ronaldo kupiga goli mbili na hivyo kuisaidia Real Madrid kupita hatua ya 16 bora.
Matokeo ya ujumla ya Real Madrid kwenye hatua ya 16 bora;
5-0 v FC Bayern Munich, 2013/14
3-4 v Borussia Dortmund, 2012/13
3-3 v FC Bayern Munich,
1-3 v FC Barcelona, 2010/11
3-4 v Juventus, 2002/03
3-1 v FC Barcelona, 2001/02
1-3 v FC Bayern Munich, 2000/01
3-2 v FC Bayern Munich, 1999/2000
2-0 v Borussia Dortmund, 1997/98
1-6 v AC Milan, 1988/89
1-1 v PSV Eindhoven, lost on away goals, 1987/88
2-4 v FC Bayern Munich, 1986/87
2-1 v FC Inter Milan, 1980/81
3-5 v Hamburger SV, 1979/80
1-3 v FC Bayern Munich, 1975/76
1-3 v AFC Ajax, 1972/73
3-4 v Manchester United FC, 1967/68
2-1 v FC Inter Milan, 1965/66
8-1 v FC Zürich, 1963/64
6-0 v R. Standard de Liège, 1961/62
6-2 v FC Barcelona, 1959/60
2-1 v Club Atlético de Madrid, 1958/59
4-2 v Vasas SC, 1957/58
5-3 v Manchester United FC, 1956/57
5-4 v AC Milan, 1955/56
Barcelona yatinga fainali klabu bingwa Ulaya
Barcelona yatinga fainali klabu bingwa Ulaya
Barcelona imefuzu kucheza fainali ya klabu bingwa Ulaya licha ya kupoteza mchezo wake wa nusu fainali ya pili dhidi ya Bayern Munich kwa kufungwa goli 3-2 mchezo uliopigwa kwenye dimba la Alianz Arena, Ujerumani.
Bayern Munich ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la mapema kupitia kwa beki wao Medhi Benatia lakini Neymar Jr alifunga magoli mawili na kuifanya Barcelona imalize kipindi cha kwanza ikiwa mbele kwa magoli 2-1.
Kipindi cha pili Bayern ilibadilika na kucheza mpira wa pasi nyingi uliowachanganya wapinzani wao na kufanikiwa kusawazisha goli kupitia kwa mshambuliaji wao Robert Lewandowski kabla ya Thomas Muller hajafunga goli la tatu na la ushindi kwa upande wa Bayern Munich.
Ushindi huo haukuisaidia Bayern kwasababu tayari ilishapoteza mchezo wake wa kwanza ikiwa ugenini kwa kukubali kipigo cha goli 3-0 kwenye uwanja wa Nou Camp juma lililopita, leo ilikuwa inahitaji ushindi wa goli 3-0 ili mchezo uongezwe dakika 30 au ushindi wa goli 4-0 ili ifuzu moja kwa moja.
Matokeo hayo yanaifanya Barcelona kusonga mbele kwenye hatua ya fainali kwa wastani wa magoli 5-3 na inasubiri mshindi wa mechi kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus ili kujua ni timu ipi kati ya hizo mbili watakutana nayo kwenye mchezo wa fainali.
Majanga yaikumba Nepal, watu wengine 40 wafa kwa tetemeko
Majanga yaikumba Nepal, watu wengine 40 wafa kwa tetemeko
Mvua kubwa iliyoambatana na tetemeko kubwa nchini Nepal imesababisha watu 40 kufariki dunia. Wakuu nchini humo wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko hilo jipya , imepanda na kufikia zaidi ya watu 40.
Wakati huo huo helkopta ya kikosi cha majini ya Marekani,ambayo ilikuwa ikifanya kazi ya kusaidia kusambaza huduma za kibinaadamu nchini Nepal, haijulikani.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa, ndani ya helkopta hiyo kulikuwa na watu nane,miongoni mwao, sita ni askari wa kikosi cha majini cha Marekani na askari wawili wenyeji wa jeshi la Nepal.
Maofisa wa serikali wa Marekani wamesema kwamba helkopta hiyo ilikuwa maeneo ya jirani na kijiji cha Charikot, ambacho kiliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi.
Rais Nkurunzinza ”apinduliwa” Burundi
Rais Nkurunzinza ”apinduliwa” Burundi
Meja Generali Niyombareh aliyetimuliwa nchini Burundi ametangaza rasmi kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi.
Amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
Wakati akitangaza uamuzi huo Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la nchini Burundi.
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpito.
Habari kutoka Burundi zimebainisha kuwa raia wengi wamejitokeza barabarani huku wakishangilia kauli hiyo ya ”Mapinduzi”.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
Bungeni: Pinda ataja sababu za mauaji ya Albino
Bungeni: Pinda ataja sababu za mauaji ya Albino
Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amezitaja sababu zinazopelekea kukithiti kwa mauaji ya Albino nchini Tanzania yaliyopelekea watu wenye aualbino kuuawa pamoja na kupoteza viungo mbalimbali vya mwili.
Akizungumza katika kikao cha bunge la Bajeti 2015/2016 leo mjini Dodoma Mh. Pinda amesema mwaka 2010 kulikuwa na tukio moja la mauaji ya albino, 2011 hapakuwa na tukio la mauaji, 2012 tukio moja, 2013 tukio moja, 2014 matukio manne na mwaka 2015 tukio moja.
Takwimu hizo zinaonesha kwamba 2006-2015 jumla ya wenye ulemavu wa ngozi 43 wameuawa kutokana na vitendo hivyo vya ukatili. Suala hilo limesababisha watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na familia zao kuishi kwa hofu na mashaka kushindwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
Vitendo hivyo, vimeleta taswira isiyo nzuri kwa nchi ya Tanzania kwa kuwa watu wengi nje ya nchi wana amini watanzania wananishi kwa upendo na amani.
Katika kupambana na kuatili huo,jumla ya watuhumiwa 181 walikamatwa na kuhojiwa kati ya mwaka 2006 hadi 2015, kati yao wautuhumiwa 133 wamefikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi za mauaji na 46 kwa makosa ya kujeruhi.
Wathumiwa 13 wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa na mtuhumiwa 1 amehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kosa la kujeruhi na watuhumiwa 73 wameachiwa huru na mahakama kwa kukosa ushahidi. Wathumiwa 6 hawajakamatwa na upelelezi wa kesi kumi bado unaendelea. Watuhumiwa wawili waliuawa na wananchi wenye hasira kali.
Akizungumzia chanzo cha mauaji hayo Mh. Pinda amesema chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina, huku baadhi ya watu wakiamini viungo hivyo vitawapa mafanikio au vyeo, mali au utajiri.
Amesisitiza kuwa utajiri hauwezi kupatikana kwa njia haramu kama hizo, utajiri unapatikana kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na sio vinginevyo huku akiyataka mashirika ya dini kuwaelimisha wananchi dhidi kuondoa imani potofu.
Monday, 4 May 2015
Mayweather apewa ushindi
Mayweather apewa ushindi
Floyd Mayweather amemshinda Manny Pacquiao kwa pointi kwenye pambano ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa masumbwi kote duniani, pambano hilo limemalizika muda mfupi kwenye ukumbi wa MGM Grand Las Vegas, Marekani.
Kama ilivyotegemewa na watu wengi, Pacquiao alirusha makonde mengi kwa mpinzani wake lakini Mayweather aliweza kuhimili mikikimikiki ya makonde hayo ambayo yalionekana kuwa mepesi kwake.
Mayweather aliwashawishi majaji wa pambano hilo kwa kutupa makonde machache lakini mazito yaliyo muingia sawasawa mpinzani wake. Majaji wa mpambano huo wamempa Mayweather ushindi wa pointi 118-110, 116-112,116-112.
Hivi ndivyo mambo yalivyo kua.
Chelsea bingwa Uingereza
helsea bingwa Uingereza
Chelsea ndio mabingwa wapya wa ligi kuu nchini Uingereza mara baada ya kuichapa timu ya Crystal Palace kwa bao 1-0 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Stamford bridge jijini London.
Bao la Chelsea limefungwa na Eden Hazard katika dakika ya 45 kwa kichwa baada ya hapo awali kipa kupangua mkwaju wa penati kasha Hazard baadae kuunganisha kwa mara nyingine tena.
Ushindi huo umeipeleka Chelsea pointi 16 zaidi ya Arsenal ambao hata hivyo wana michezo mitano kibindoni.
Lakini hata Arsenal na Man City wakishinda michezo yao yote iliyosalia bado hawataweza kuwafikia Chelsea.
Hii ni mara ya tatu sasa kwa Mourinho kushinda kombe hilo akiwa na Chelsea na ni mara ya kwanza kwake tangu arudi tena klabuni hapo mwaka 2013.
Chelsea sasa watakuwa wamechukua kombe hilo kwa mara ya tano tangu klabu hiyo kuanzishwa.
Kopunovic: Simba ni timu bora Tanzania
Kopunovic: Simba ni timu bora Tanzania
“Niliiandaa vizuri timu yangu, Azam FC ni mabingwa na bado nawaona ni mabingwa, ni timu ngumu, nina furaha sana kwasababu nilikuwa na msongo wa mawazo, sio mimi tu, kila mtu ndani ya timu”, amesema Kopunovic
“Nina furaha sana, najivunia sana kuwa timu yangu ndio bora nchini Tanzania, tulimfunga Yanga, tumemfunga Azam, nadhani hakuna swali tena ni timu gani bora Tanzania”, Kopunovic alitamba.
‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba wamefikisha pointi 44 katika nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 25, pointi moja nyuma ya Azam FC waliopo nafasi ya pili kufuatia kushuka dimbani mara 24.
Magoli ya Ibrahim Ajib na Ramadhani Singano ‘Messi’ yalitosha kuwapa Simba ushindi dhidi ya Azam FC katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa jana kwenye uwanja wa Taifa. Goli pekee la Azam lilifungwa na kiungo Mudathir Yahya dakika ya 58.
Ili Simba wamalize ligi wakiwa nafasi ya pili, wanahitaji kushinda mechi yao ya mwisho Mei 9 dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Taifa, halafu Jumatano Azam wafungwe na Yanga na kutoa sare mechi ya mwisho dhidi ya Mgambo JKT.
Share
Habari picha, Simba walivyoitandika Azam
Habari picha, Simba walivyoitandika Azam
Jana kikosi cha ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba kilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Hizi ni picha zinazoonesha baadhi ya matukio mbalimbali yaliyookea kwenye uwanja wa Taifa wakati wa mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC.
Wananchi 700 waokolewa kambi ya Boko Haram
Wananchi 700 waokolewa kambi ya Boko Haram
Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaokoa zaidi ya watu mia saba katika kipindi cha wiki moja iliyopita wakati wa mapigano makali yanayoendelea dhidi ya Boko Haram. Mateka mia tatu wameokolewa kutoka msitu wa Sambisa na kupelekwa katika kambi ya serikali.
Wakizungumzia mateso waliyoyapata kutoka kundi la Boko Haram baadhi ya mateka wamesema kwamba baadhi yao waliuawa kwa kupigwa mawe na wapiganaji wa Boko Haram wakati jeshi lilipokaribia kuwaokoa.
Mwanamke mmoja ambaye alijifungua akiwa mateka ameelezea namna wapiganaji hao walivyomkata koo mumewe wake mbele yake, kabla mwanamke huyo kutenganishwa na watoto wake wengine watatu.
Katika hatua nyingine wengi wa wananchi waliokolewa katika kambi ya serikali imebainika kuwa wengi wa watoto waliokolewa walikuwa wanaugua utapiamlo mkali.
Mgomo wa mabasi waitikisa nchi
Mgomo wa mabasi waitikisa nchi
Mgomo mkubwa wa vyombo vya usafiri unaendelea hivisasa katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania na kusababisha adha kubwa kwa wananchi pamoja na abiria mbalimbali.
Habari kamili itakujia hivi punde, endelea kutembelea mtandao wa Hivisasa
Ugaidi: Watu 5 wajeruhiwa kwa Bomu kwenye sherehe za mei mosi
Ugaidi: Watu 5 wajeruhiwa kwa Bomu kwenye sherehe za mei mosi
Bomu hilo liliwajeruhi watu hao walipokuwa kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Msolwa Ujamaa, Kata ya Sanje ,wilayani Kilombero, mkoani Morogoro
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe alithibitisha kutokea tukio hilo na kusema tukio hilo lilitokea majira ya saa 2:00 usiku wa Mei Mosi mwaka huu eneo la Kijiji cha Sanje.
Alisema vijana wawili wanaotuhumiwa kurusha mlipuko huo baada ya kuwajeruhi watu hao watano, walifanikiwa kukimbia kutoka eneo la tukio na jeshi la Polisi inaendelea kuwasaka ili sheria ichukue mkondo wake.
Kwa mujiu wa walioshuhidia tukio hile wamebainisha kwamba vijana wawili wasiofahamika walikamatwa katika eneo la sherehe hizo lakini kabla ya kupelekwa kituoni , vijana hao walifanyiwa upekuzi na askari wa mgambo, Thomas Manjole(54) ,mkazi wa Msolwa na walibainika kuwa na bomu.
Inadaiwa kuwa vijana hao walilitoa bomu hilo kiunoni na kulirusha kwenye gari la halmashauri ambalo linatumiwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Bomu hilo lilipolipuka likamjeruhi dereva wake aliyekuwa ndani ya gari pamoja na wengine wanne akiwemo askari mgambo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye hakuwemo ndani ya gari aliwataja majeruhi hao ni dereva wake ,askari mgambo alikuwa akiwapekuwa vijana hao, Amos Msopole(29) na Azama Naniyunya(59) wote wakazi wa Kijiji cha Msolwa Ujumaa.
Hili ni tukio la pili kutokea mkoani Morogoro kufuatia lile lililotokea siku kadhaa zilizopita ambapo jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na mabomu pamoja na vifaa vya milipuko msikitikiti.
Subscribe to:
Posts (Atom)