Rais Kenyatta Atumbua Jipu, Amsimamisha Kazi Jaji
Tarehe February 23, 2016
Rais Uhuru Kenyatta amemsimamisha kazi Jaji wa Mahakama ya juu aliyetuhumiwa kuchukua hongo katika kesi kuhusu kuchaguliwa kwa gavana wa Nairobi.
Rais Kenyatta amemsimamisha kazi Jaji Phillip Tunoi na akateua jopo la kuchunguza madai dhidi yake, kwa mujibu wa mapendekezo ya Tume ya Huduma za Mahakama.
Jaji adaiwa kupokea rushwa ya $2m Kenya
Jopo la kumchunguza Jaji huyo litaongozwa na Jaji Sharad Rao ambaye ndiye mwenyekiti wa Bodi ya Kuwachunguza Majaji na Mahakimu.
Wanachama wengine wa jopo hilo ni Jaji Roselyn Korir, Jaji Mstaafu Jonathan Havelock, Judith Guserwa, James Kaberere Gachoka, Abdirashid Abdullahi Hussein na George Munji Wakukha.
Jaji Tunoi amekanusha madai dhidi yake.