IGP Atangaza Operesheni Kamata Bodaboda
Tarehe February 20, 2016
Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Ernest Mangu amewaagiza makamanda wa polisi nchini kuendesha operesheni kali ya kuwachukulia hatua za kisheria waendesha bodaboda wasiotii sheria za usalama barabarani.
Akizungumza na wakuu wa polisi, IGP Mangu alisema makosa yatakayosababisha waendesha bodaboda kukamatwa ni pamoja na kubeba abiria zaidi ya mmoja, kupita katika taa nyekundu na kutokuvaa kofia ngumu.
Alisema waendesha bodaboda wamekuwa wakikaidi kufuata sheria za barabarani, lakini sasa mwisho wao umefika kwani jeshi la polisi halitavumilia vitendo vyao tena.
IGP Mangu amesisitiza pia jeshi la polisi kuwakamata waendesha bodaboda wenye makosa tu bila uonevu.