Saturday, 20 February 2016

Tume Ya Vyuo Vikuu Yafuta Matawi Ya St. Joseph

Tume Ya Vyuo Vikuu Yafuta Matawi Ya St. Joseph

Tarehe February 19, 2016
Profesa Yunus Mgaya, Katibu Mtendaji wa TCU
Kaimu mtendaji wa TCU, profesa Yunus Mgaya
Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufuta vibali vilivyoanzisha vyuo vikuu vishiriki vya sayansi ya kilimo na teknolojia na chuo kikuu kishiriki cha teknolojia ya habari tawi la songea vinavyoendeshwa na chuo kikuu cha mtakatifu Joseph (St.Joseph) baada ya kukiuka taratibu za uendeshaji.
Kaimu mtendaji wa TCU, profesa Yunus Mgaya amesema mara kwa mara tume yake imekua ikikitaka chuo kikuu cha Mt. Josefu kutoa elimu inayokidhi viwango vya ubora vilivyowekwa na TCU katika kampusi za Songea lakini kimekua kikikiuka maagizo hayo.
“Tume imejiridhisha kuwa vyuo hivyo havitoi elimu nzuri na wanaoathirika zaidi na elimu hiyo ni wanafunzi ndio maana tumeamua kufuta kabisa vibali vilivyoanzisha vyuo hivyo,” alisema.
Vilevile TCU imeidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote 2,046 waliokuwa wanasoma chuoni hapo kwa gharama za chuo cha Mt. Joseph.
Profesa Mgaya amewaarifu wanafunzi wanaosoma katika vyuo hivyo kuwa watahamishiwa katika vyuo vingine ambavyo vinatoa programu sawa na zilizokuwa zinatolewa vyuoni huko.

clouds stream