Friday, 5 February 2016

Magufuli ‘Awatega’ Wawekezaji

Magufuli ‘Awatega’ Wawekezaji

Tarehe February 5, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa eneo la Magole mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa eneo la Magole mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kwamba wawekezaji wote waliotelekeza Mashamba na Viwanda walivyouziwa na serikali waanze kuviendeleza kabla ya serikali haijawanyang’anya na kuwagawia wanaoweza kuviendesha
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake njiani, wakati akisafiri kwa gari kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma.
Amesema mkoa wa Morogoro ulikuwa na viwanda vingi na mashamba mengi makubwa ambayo kama waliouziwa wangeyaendeleza, yangezalisha ajira na kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani na Mazao ya kilimo.
Ameongeza kuwa inashangaza waliouziwa mashamba na viwanda hivyo wameamua kuvitelekeza ama kubadilisha matumizi, huku wengine wakitumia rasilimali hizo kuombea mikopo katika mabenki jambo ambalo serikali yake haitalikubali.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekagua kipande cha barabara kuu ya Morogoro – Dodoma kilichoharibiwa na maji ya mvua katika eneo la Kibaigwa Mkoani Dodoma, na kujionea kazi za ukarabati zinazofanywa na wakala wa barabara nchini (TANROADS).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa.

clouds stream