BAKWATA Yabariki Marudio Ya Uchaguzi Z’bar
Tarehe February 2, 2016
Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) limeunga mkono kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar Machi, 20 mwaka huu na kuwaomba wazanzibari kuwa na utulivu kwani hakuna namna nyingine ya kumaliza mkwamo wa kisiasa visiwani humo.
Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, sheikh Alhad Mussa Salum amewaambiwa waandishi wa habari kuwa hakuna namna nyingine ya kumaliza mkwamo wa kisiasa visiwani humo isipokuwa kurudia uchaguzi kama ilivyopangwa na tume ya uchaguzi ya Zanzibar.
Pia Sheikh Saluma amesema amepokea barua kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha Uamsho alie gerezani, sheikh Farid Hadi Ahmed ambaye amesisitiza umuhimu wa kurudia uchaguzi visiwani Zanzibar mapema ili Wazanzibari waendelee na shughuli zao za kawaida.
Vilevile sheikh huyo amekiomba chama cha Wananchi (CUF) ambacho kimeshatangaza kususia uchaguzi huo, kiache kususia uchaguzi huo bali kijipange na kushiriki upya.