Fomu Za Kupigia Kura Zatua Z’bar, Jina La Maalim Seif Lipo
Tarehe March 12, 2016
Fomu za kupigia kura katika uchaguzi wa marudio zimewasili Visiwani Zanzibar na kupokewa na watendaji mbalimbali wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), wakiongozwa na mkurugenzi wake, Salim Kassim katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Kuwasili kwa fomu hizo ni maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Machi 20 ambapo jumla ya karatasi 5,385 ndizo zilizowasili.
Kassim alisema fomu hizo zimechapishwa katika kiwanda cha Unprint cha Durban, Afrika Kusini na ziliwasili hapo kwa ndege yenye Na EW-364TG ya nchi hiyo. Alisema karatasi hizo pamoja na vifaa vingine vitasambazwa vituoni Machi 18, mwaka huu.
Aliongeza katika fomu hizo za kupigia, yapo pia majina ya wagombea wote tisa wa vyama vya upinzani waliokwishatangaza kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio.
Huku jina la Miongoni mwa wagombea hao ni Maalim Seif Sharif Hamad wa CUF, ambaye ametangaza kujitoa.
Vyama vilivyotangaza kususia uchaguzi ni CUF Chaumma, Chama cha Kijaamii (CCK), APPTMaendeleo, ACT-Wazalendo, Jahazi Asilia, Demokrasia Makini, NRA na SAU.
Kassim alipotakiwa kueleza sababu za ZEC kuchapisha fomu za kura zenye wagombea waliotangaza kususia uchaguzi huo wa marudio, alijibu kuwa yeye si msemaji.
Akizungumzia gharama za uchaguzi huo wa marudio, mhasibu wa ZEC, Yussuf Ali Hassan alisema utagharimu Sh4.5 bilioni wakati wa mwaka jana uligharimu Sh5.3 bilioni