Monday, 14 March 2016

Treni Reli Ya Kati Yaanza Kupiga Mzigo Tena

Treni Reli Ya Kati Yaanza Kupiga Mzigo Tena

Tarehe March 14, 2016
reni ya Mizigo ikiwa tayari kuanza safari katika eneo la Kidete Wilayani Kilosa, kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa eneo hilo, uliodumu kwa takriban miezi miwili na hivyo kurudisha mawasiliano ya reli kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
reni ya Mizigo ikiwa tayari kuanza safari katika eneo la Kidete Wilayani Kilosa, kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa eneo hilo, uliodumu kwa takriban miezi miwili na hivyo kurudisha mawasiliano ya reli kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Huduma ya usafiri wa reli ya kati iliyokuwa imesimama kwa takribani miezi miwili sasa imerejea katika hali yake ya kawaida kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa reli hiyo katika eneo la Kidete Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo baada ya kukagua na kuridhika na ukarabati uliofanywa katika maeneo ya Magulu, Munisagara, Mzaganza na kidete Wilayani Kilosa.
“Hakikisheni mnailinda reli hii kwa manufaa yenu na ya Taifa, leo hii reli iko vizuri na treni ya kwanza kutoka Dar es Salaam kwenda bara itapita na kumaliza changamoto ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi wanaotumiia reli hii,” amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo ya Kilosa, Magulu, Munisagara, Mzaganza, Kidete, Godegode na Gulwe ambao maeneo yao yanakabiliwa na mafuriko ya mto Mkondoa kuacha kilimo cha kuelekeza maji kwenye reli bali washirikiane na Serikali kudhibiti maji hayo kwenda kwenye hifadhi ya reli.
Amesema Shirika la Reli Tanzania (TRL) litaendelea kuhakikisha kuwa treni inayopita kwenye reli ya kati inapata mzigo mwingi wa kusafirisha kutoka bandarini za Tanga na Dar Es Salaam kuelekea mikoa ya Mwanza, Kigoma na Mpanda na hivyo kuwataka wafanyabiashara watumie fursa hiyo ili kupunguza mzigo unaosafirishwa kwa njia ya barabara.
Pia Profesa Mbarawa ametembelea bwawa la Kidete linaloelezwa kuwa chanzo cha mafuriko pindi linapojaa wakati wa mvua za vuli na masika katika mikoa ya Dodoma na Iringa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, John Henjewele amemhakikishia Profesa Mbarawa kuwa ofisi yake itafuatilia kwa karibu malalamiko ya wananchi wanaoishi karibu na reli ya kati ili kuyapatia ufumbuzi na kuwataka wananchi hao kuitumia fursa ya kuwa karibu na reli kunufaika kiuchumi.
Takribani Shilingi million 926 zimetumika katika ukarabati wa reli hiyo kufuatia uharibifu uliotokea mwezi Januari na kukata mawasiliano ya reli kati ya mikoa ya Dodoma na Morogoro na kusababisha safari za treni kutoka bara kuishia Dodoma.

clouds stream