Thursday, 10 March 2016

TRA Yaitaja Z’bar ‘Ngome’ Ya Wakwepa Kodi

TRA Yaitaja Z’bar ‘Ngome’ Ya Wakwepa Kodi

Tarehe March 10, 2016
tanga
Shehena ya bidhaa zisizolipiwa kodi kutoka Zanzibar ilipokamatwa mapema mwaka huu
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema visiwa vya Zanzibar vinaongoza kwa kutumika na wafanyabiashara wasiowaaminifu wanaokwepa kodi kwa kutumia mianya mbalimbali iliyopo visiwani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, takwimu zinaonyesha uwapo wa wafanyabiashara wanaopitisha bidhaa za magendo kwa njia ya panya kati ya mianya 509, Zanzibar inaongoza kwa kuwa na mianya 422,  huku Tanzania Bara ikiwa na mianya 87.
Alisema hali hiyo isipodhibitiwa haraka itaendelea kuisababishia serikali hasara na kwamba licha ya bandari ya Dar es Salaam kuchangia mapato kwa kudhibiti wafanyabaishara wanaokwepa kodi, bado kuna haja ya kuandaliwa mazingira rafiki yatakayowabana wakwepa kodi wanaotumia njia hizo za panya.
“Tusiridhike na kiwango cha kodi tunachokusanya kwa sasa, ila iwekezwe nguvu kubwa kumaliza tatizo hilo,” alisema Kidata.
Kidata amesema hali ya ukwepaji kodi imeilazima mamlaka yake kufanya operesheni mbalimbali katika mianya ambayo imetambulika na kufanikiwa kukamata bidhaa nyingi kwa kushirikiana na jeshi la polisi.

clouds stream