Maalim Seif Akana Kuzungumza Siasa Na Shein
Tarehe March 12, 2016
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Hamad amesema mikutano yake ya hivi karibuni na Rais wa Tanzania John Magufuli na yule wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein haikua na agenda yoyote ya kujadili hali ya siasa inayoendelea visiwani Zanzibar.
Maalim Seif ameyasema hayo baada ya kuwepo na tetesi kuwa ugeni wa maraisi hao ulilenga kuzungumzia uchaguzi wa marudio wa Zanzibar ambao utafanyika Machi 8 mwaka huu.
Alisema Rais Magufuli na Shein walikwenda kumjulia hali kibinadamu tu hivyo kuwataka wazanzibari na wafuasi wa CUF kutokuwa na hofu yoyote.
Ikumbuke kwamba CUF imegomea uchaguzi wa marudio Zanzibar ikishinikiza Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itangaze mshindi wa matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
Maalim Seif amepumzishwa katika hospitali ya Serena baada ya kuugua akiwa safarini kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam.