Friday, 11 March 2016

Mnada Wa Pugu Waingiza Mil 600 Kwa Wiki 12

Mnada Wa Pugu Waingiza Mil 600 Kwa Wiki 12

Tarehe March 11, 2016
mwigulu
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Chemba alipotembelea mnada wa Pugu mapema mwaka huu
Wizara ya Kilimo, Migugo na Uvuvi imekusanya mapato ya shilingi milioni 676.4 kuanzia Disemba 19, 2015 hadi Machi 9, 2016 katika mnada wa Pugu baada ya kuweka mikakati bora ya kukusanya mapato katika mnada huo.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara, Mkurugenzi wa Huduma za mifugo,  Abdu Hayghaimo amesema hapo awali wafanyabiashara walikuwa wakikwepa kupeleka mifugo yao ili kukwepa ushuru wa serikali.
Makusanyo hayo yameongezeka baada ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nash kuagiza Idara za Huduma za Mifugo na uzalishaji na masoko kufanya doria ili kuhakikisha kwamba mifugo yote ambayo inanunuliwa kwenye minada ya awali inapelekwa kwenye mnada wa upili uliopo Pugu Dar es salaam ili kukaguliwa afya zao na kutolewa ushuru.
Hayghaimo amesema baada ya kuanza kazi za doria na kudhibiti maeneo yote kuanzia machinjioni hadi kwenye mnada wa pugu, mapato ya Serikali kwenye mnada huo yamepanda kwa wiki kutoka wastani wa sh mil 24 mwezi December 2015 kwa wiki hadi  sh mil 61 kwa wiki mwezi March 2016.
“Hii inaonesha kwamba kabla ya doria kulikuwa na upotevu mwingi wa mapato ya Serikali kwenye mnada wa Pugu na kwenye machinjio ya Mkoa wa Dar es salaam.”

clouds stream