Tarehe Aug, 4 2016
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam imewafutia Mashtaka ya kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni 30 yaliyokuwa yanawakabili wabunge Kangi Lugola wa Mwibara, Victor Mwambalaswa wa Lupa na Murad Sadiq wa Mvomero.
Hatua hiyo inakuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP, kusema hana nia ya kuendelea na Mashtaka dhidi ya wabunge hao hivyo kuiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia mashtaka wabunge hao