Tarehe August 1, 2016
Mohammed Dewji akisalimiana na mmoja wa wadau kwenye jukwaa kuu wakati wa tamasha la Simba Day. Mfanyabiashara bilionea Mohamed Dewji baada ya jana kufanikiwa kushinda imani ya wanachama wa simba na kupewa idhini ya kuendeleza timu hiyo leo ameibuka na kuwashukuru wanachama wa Simba kwa uamuzi huo na kupinga hoja ya kuwa hajazungumza na viongozi wa klabu hio.
Dewji alianza kwa kuwashukuru wanachama wa Simba kwa kupitisha ajenda ya mabadiliko licha ya viongozi kutowasilisha taarifa ya maoni ya kamati iliyoteuliwa kukusanya maoni ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji. ” Mimi Mohamed Dewji nashukuru sana wanachama wa Simba kwani wamevuja damu, jasho kwa ajili ya Simba, nasema nitakuwa nao bega kwa bega. ”
” Kwa namna moja au nyingine, kuna hoja zimeniumiza na zilikuwa za upotoshaji na nimeona ni vyema kuziongelea kwa undani. ” ” Kuna hoja ya kwanza viongozi wanasema natangaza kwenye vyombo vya habari na sisihatujawahi kukutana. Leo labda niwe wazi zaidi, nishakutana na Rais wa Simba , Evan Aveva zaidi ya mara tatu. Alikuja na wajumbe wa kamati kuu.”
Dewji pia amefafanua hoja ya kutotuma ofa yake kwa maandishi na kudai alikuwa anasubiria ridhaa ya wanachama. Kwa kuwa wanachama wameshatoa ridhaa ametuma rasmi barua kwa viongozi wa Simba.
“leo asubuhi nimeandika barua kwenda kwa Rais wa Simba bahati mbaya ofisi yake imefungwa, ikifunguliwa tu barua yangu ya kwanza”.
” Ni dhahiri kwamba baadhi ya viongozi wanaoongozwa na Rais Evans Aveva hawataki mabadiliko lakini nashukuru wanachama wananiunga mkono”.