Thursday, 11 August 2016

Bodi Ya Mikopo Yapata Bosi Mpya.

Tarehe August 12, 2016 
imagesV 1

Serikali imemteua Abdul­Razaq Badru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).

Badru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na George Nyatage aliyefurumushwa kazi pamoja na vigogo wengine watatu ikiwa ni miezi sita tu tangu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako awatumbue vigogo hao kwa ufisadi katika bodi hiyo na kusababisha upotevu wa mamilioni ya fedha.

Uteuzi wa Bosi huyo mpya ulioanza tangu Julai 20, mwaka huu umetangazwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya HESLB, Prof. Anselm Lwoga na kudai kuwa kiongozi huyo mpya ameteuliwa kwa mujibu wa vifungu namba 10 (1) na 11 (1) na (2) vya Sheria ya HESLB namba 9 ya mwaka 2014.

Kifungu hicho kinampa mamlaka Prof. Ndalichako kumteua Mkurugenzi Mtendaji aliyependekezwa na Kamati Maalum ya Bodi ya Wakurugenzi.

Kabla ya uteuzi huo, Badru alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Ifakara.

clouds stream