Wednesday, 31 August 2016

Viongozi Chadema Kuripoti Polisi Septemba Mosi.

Tarehe August 31, 2016
lowassa_mboweV 1

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward Lowassa na viongozi wengine waandamizi wameitwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwenda kuripoti kesho Septemba Mosi.

Hatua hiyo inatokana na viongozi hao kukamatwa juzi, baada ya kufanya kikao cha ndani cha Kamati Kuu, katika Hoteli ya Giraffe, Jijini Dar es Salaam na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati ambapo walihojiwa kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Mbali na Mbowe na Lowassa, viongozi wengine wa Chadema waliokamatwa na kutakiwa kwenda Polisi kesho ni Katibu Mkuu, Vincent Mashinji, Naibu wake, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Said Issa Mohammed.

Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amesema ni kweli wametakiwa kwenda polisi Septemba Mosi kuripoti baada ya kukamatwa na kuhojiwa wakituhumiwa kukiuka maagizo ya polisi.

“Maandamano yatakuwepo kama yalivyopangwa hapo awali kwani maandalizi yote yamekwishakamilika lakini viongozi hao wanaweza kwenda polisi kwanza au wakaanzia kwenye maandamano kisha wakaenda Polisi kuripoti,” amesema Makene.

clouds stream