Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
Rais Dkt.John Pombe Magufuli amesema Serikali ya Morocco inatarajia kuisaidai Tanzania vitu 3 katika kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Akizungumza leo katika Hafla ya utiaji saini Ikulu jijini Dar es salaam leo Rais Magufuli alisema kwamba amemuomba Mfalme wa Morocco Mohammed VI kujenga Msikiti mkubwa katika Jiji la Dar es salaam amekubali kazi ya kuujenga Msikiti huo.
Rais Magufuli amemuomba Mfalme huyo kujenga uwanja mkubwa wa Mpira wa Kisasa Makao makuu ya nchi mjini Dodoma ambao utakuwa na thamani ya dola milioni 80 hadi 100 na Mfalme huyo pia ameahidi kuujenga uwanja huo.
Rais Magufuli amesema kwa mategemeo yake uwanja huo utakuwa mkubwa zaidi kuliko uwanja wa Mpira wa jijini Dar es salaam ambao ndio mkubwa kwa kuliko uwanja mwingine wowote hapa nchini.
Kwa upande wa mambo mengine Rais Magufuli amesema wamekubaliana kufanya mafunzo ya ulinzi kati ya nchi hizo mbili za Tanzania na morocco ambapo zaidi ya Maaskari 150 watakwenda nchini Morocco wiki ijayo kwenda kujifunza.
Katika ziara yake nchini Tanzania Mfalme wa Morocco na Mawaziri kutoka nchini humo wametiliana saini mikataba takribani 21.