Monday, 14 November 2016

Waziri Mkuu Congo DRC Ajiuzulu

Waziri mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo.
V 2
Waziri mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo.
Waziri mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, amejiuzulu na kutoa fursa ya kuteuliwa mrithi wake kuongoza serikali ya mpito.
Kujiuzulu kwa bwana Ponyo ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita kati ya serikali ya Rais Joseph Kabila na baadhi ya vyama va upinzani ya kuhairisha uchaguzi wa urais hadi mwezi Aprili mwaka 2018.
Wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa mhula wake wa mwisho.
Vyama vikuu vya upinzani vinakataa kuhairishwa kwa uchaguzi vikisema kuwa hiyo ni njama ya Rais Kabila ya kusalia madarakani.
Kufuatia kuziuzulu kwa Waziri Mkuu,Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu na bwana Ponyo.

clouds stream