Wanasayansi wamevumbua njia mpya ya kupima HIV ambayo itahitaji tu kuchomeka kifaa kwenye kompyuta kama unavyochomeka USB Flash.
Watafiti wanadai kuwa kifaa hicho kinaweza kubaini virusi kwenye tone la damu na kutoa majibu yanayoweza kusomwa kwenye laptop. Kifaa hicho kinaweza kutoa majibu ndani ya dakika 30. kimetengenezwa na timu ya Imperial College London na kampuni ya DNA Electronics.
Hutohitaji kwenda hospitali kujua afya yako, kifimbo hiki cha USB kinaweza kukupa majibu iwapo unamaambukizo au lah!