Chanjo mpya dhidi ya virusi vya ukimwi na ukimwi inatarajiwa kufanyiwa majaribio hii leo nchini Afrika Kusini.wanasayansi wanaeleza kwamba itakuwa kliniki kubwa na ya aina yake katika nchi ambayo ugonjwa wa ukimwi umeota miziz.
Taasisi ya kitaifa ya Afya nchini Marekani, ambayo inafadhili jaribio hilo, imeeleza kwamba zaidi ya watu elfu moja hupata maambukizi mapya kila siku nchini humo.
Utafiti huo umepewa jina HVTN 702 una lengo la kuwafikia zaidi ya watu 5000 wanaojishirikisha na ngono wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi kwa wanaume na wanawake nchini Afrika Kusini.
Idadi hiyo imeahidiwa kupata sindano tano kwa mwaka. Chanjo hiyo ilikwisha fanyiwa majaribio mwaka 2009 nchini Taniland na kuonekana inaouwezo wa kuzuia maambukizi kwa asilimia thelathini na moja katika kipindi cha miaka mitatu.
Wanasayansi bado wanalo tumaini kwamba kwa asilimia hamsini na zaidi chanjo hiyo inao uwezo wa kuonesha mafanikio nchini Afrika Kusini kwa watu wanaokadiriwa kufikia milioni saba ambao wanaishi na virusi vya ukimwi na ukimwi.
Matokeo ya utafiti wa chanjo hiyo yanatarajiwa kutolewa hadharani katika kipindi cha miaka minne ijayo.