Rais wa Colombia Juan Manuel Santos na kiongozi wa kundi la FARC Rodrigo Lodono maarufu kama Timochenko, wametia saini makubaliano ya amani huko Bogota ambapo inatarajiwa itamaliza malumbano yaliyodumu kwa takribani nusu karne.
Makubaliano ya kwanza yalipingwa mwezi uliopita kwa kura za maoni.
Wapinzani walipinga na kusema kwamba mkataba huo ulikuwa hauna manufaa kwao.
Wiki ijayo makubaliano yatawasilishwa bungeni kwa uchambuzi zaidi ambapo muungano wa serikali unawingi wa viti.
Upinzani unaongozwa na Alvaro Uribe aliyekuwa Rais ambapo wataongoza maandamano wakishinikiza kuwepo kwa kura za maoni kwa mara ya pili kuhusiana na mkataba huo.