Mshambuliaji wa klabu ya Genk ya Ubelgiji na timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetoa orodha ya wachezaji watano watakaowania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika 2016, na kumuengua nyota na straika wa Tanzania, Mbwana Samatta aliyekuwemo katika orodha ya awali ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo ya heshima kubwa Afrika.
Wachezaji watano ambao sasa watamenyana kuisaka tuzo hiyo ni pamoja na Emerick Aubameyang kutoka nchini Gabon na anayekipiga katika klabu ya Borrusia Dortmund, Sadio Mane kutoka Senegal na anayekipiga katika klabu ya Liverpool, na Riyadh Mahrez kutoka Algeria na anyekinukisha katika klabu ya Leicester City.
Wengine ni pamoja na Mohamed Salah kutoka Misri na anayeichezea klabu ya Roma ya Italia na wa mwisho ni Islam Slimani kutoka Algeria na anayeichezea klabu ya Leicester City.