Saturday, 21 January 2017

Gambia: Jammeh atangaza ataondoka madarakani

Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi na Adama Barrow

Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi na Adama Barrow
img-20161130-wa0008

Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia Yahya Jammeh, anasema kuwa ataondoka madarakani baada ya kukataa kukubali kushindwa.

Katika tangazo kwenye runinga, Jammeh alisema kuwa hakuna haja ya "hata tone moja la damu" kumwagika.

Alitoa tangazo hilo baada ya mazungumzo ya saa kadha kati yake na wapatanishi wa Afrika Magharibi.

Hata hivyo hakuna taarifa zaidi kuhusu yale yaliyoafikiwa.

Bw Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Desemba na mrithi wake Adama Barrow tayari ameshaapishwa.

Bw Barrow amekuwa akiishi katika taifa jirani la Senegal kwa siku kadha.

Wanajeshi kutoka nchi za magharibi mwa Afrika ikiwemo Senegal wametumwa nchini Gambia wakitisha kumtimua Bw Jammeh madarakani.

Bw Adama Barrow, aliapishwa kuwa rais katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal Alhamisi
Bw Adama Barrow, aliapishwa kuwa rais katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal Alhamisi

Uamuzi wa Jammeh kung'atuka aliufanya baada ya kufanya mazungumzo na marais wa Guinea na Mauritania waliofika mjini Banjul Ijumaa kujaribu kumshawishi kuondoka madarakani kwa amani.

"Nimeamua leo, nikiwa na dhamiri njema, kuachia uongozi wa taifa hili kubwa nikiwa na shukrani zisizo na kikomo kwa raia wa Gambia," amesema.

"Namuahidi Allah na taifa lote kwamba masuala masuala ambayo yanatukabili kwa sasa yatatauliwa kwa njia ya amani"

Muda mfupi kabla ya Jammeh kutoa hotuba yake kwenye runinga, Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz alisema kwamba maafikiano yalikuwa yamefikiwa na kwamba Bw Jammeh angeondoka nchini humo.

Hakutoa taarifa zaidi.

Bw Jammeh alikuwa amepewa makataa ya saa sita mchana kuondoka madarakani la sivyo aondolewe kwa nguvu na wanajeshi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Makataa hayo yalimalizika saa sita mchana, wakati mazungumzo kati yake na Abdel Aziz na Rais Alpha Conde wa Guinea yakianza. Aliomba aongezewe muda hadi saa kumi saa za Gambia.

Map of The Gambia

Dalili za kwanza za kupatikana kwa maafikiano zilianza kuonekana baadaye Ijumaa wakati mmoja wa wasaidizi wakuu wa rais mpya alipomwambia mwandishi wa BBC Umaru Fofana kwamba Bw Jammeh amekubali kuachia madarakani.Bw Jammeh alikuwa awali amekubali kushindwa lakini baadaye akabadili msimamo wake na kusema hangeng'atuka akisema uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu na kasoro nyingi.

Aliwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo hayo na baadaye akatangaza hali ya tahadhari ya siku 90.

Baadaye, alihakikisha bunge la nchi hiyo linapitisha sheria ya kumruhusu kuendelea kuongoza kwa muda hadi mwezi Mei.

Tume ya uchaguzi ilikiri kwamba kulikuwa na kasoro kwenye baadhi ya matokeo yaliyotangazwa, lakini ikasema kasoro hizo hazingebadilisha ushindi wa Bw Barrow.

Bw Jammeh awali alikuwa ameappa kuendelea kuongoza hadi uchaguzi mpya ufanyike.

Mbona Senegal inaongoza kumkabili

Ecowas, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, iliipa Senegal jukumu hilo kwa sababu taifa hilo linaizunguka Gambia.

Kanali Abdou Ndiaye, msemaji wa jeshi la Senegal, amesema Ecowas iliamua kumuwekea Jammeh makataa ili kujaribu kupata suluhu ya kidiplomasia.

Wanajeshi wote wa Gambia ni takriban 2,500.

Rais Macky Sall wa Senegal akiwa na Adama Barrow
Rais Macky Sall wa Senegal akiwa na Adama Barrow awali Ijumaa

Hii inaifanya vigumu kufikiria ni vipi wanaweza kuwashinda wanajeshi wa kanda hiyo, anasema mwandishi wa BBC wa masuala ya usalama Afrika Tomi Oladipo.Nigeria imetuma ndege za kivita na ndege nyingine za kawaida, pamoja na wanajeshi 200 nchini Senegal. Wanajeshi hao walienda Senegal Jumatano asubuhi.Meli za kivita za Nigeria pia zimewekwa tayari baharini.Manowari moja iliondoka Lagos Jumanne na itakuwa na jukumu la kuwaokoa raia wa Nigeria walio nchini Gambia.Ghana pia inachangia wanajeshi.

clouds stream