Wednesday, 18 January 2017

Mhubiri aliyetabiri kifo cha Mugabe akamatwa Zimbabwe

Rais Mugabe akihutubu Februari 27, 2016

Mugabe ameongoza Zimbabwe tangu 1980
img-20161130-wa0008

Maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wamemkamata na kumzuilia mhubiri aliyetabiri kwamba Rais Robert Mugabe atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.

Pasta Patrick Mugadza alikamatwa akiwa mahakamani mjini Harare Jumatatu ambapo alikuwa ameenda kwa kesi nyingine dhidi yake, wakili wake Gift Mtisi ameambia wanahabari.

Alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuvalia bendera ya taifa

"Alikuwa amefika mahakamani kwa kesi hiyo polisi walipomkamata wakati wa mapumziko na kumfungulia mashtaka kwa sababu ya unabii huo," Bw Mtisi aliambia AFP.

"Awali alishtakiwa kwa kudunisha na kukosea heshima mamlaka ya rais lakini shtaka hilo likabadilishwa baadaye na kuwa kuwatusi watu wa asili fulani au dini fulani."

Pasta Mugadza, ambaye huhudumu katika mji wa Kariba kaskazini mwa nchi hiyo, aliandaa kikao na wanahabari wiki iliyopita ambapo alitabiri kwamba Mugabe angefariki Oktoba 17 mwaka huu.

Kumfanyia mzaha Rais Mugabe au kutoa unabii au ubashiri kumhusu ni jambo hatari nchini Zimbabwe.

Patrick MugadzaPATRICK MUGADZA
Patrick Mugadza amekamatwa mara kadha na polisi Zimbabwe

Nchini humo kuna sheria ambayo huharamisha "kudunisha mamlaka ya au kumtusi rais."

Mwaka 2015, Mugadza alikamatwa na kuzuiliwa kwa karibu mwezi mmoja baada ya kujitokeza hadharani na bango lililokuiwa na ujumbe uliomwambia Mugabe kwamba watu wamekuwa wakiteseka chini ya utawala wake.

Siku ya maadhimisho ya uhuru mwaka jana, alitoa mahubiri akiwa amejifungia kwenye boriti ya taa nje ya duka kubwa zaidi la kibiashara mjini Harare, akisema hiyo ilikuwa ishara ya raia kukandamizwa Zimbabwe.

Maandamano ya kupinga uongozi warais Mugabe Zimbabwe
Maandamano ya kupinga uongozi w arais Mugabe Zimbabwe

Rais Mugabe amekuwa madarakani tangu 1980.

Kumekuwa na uvumi kuhusu afya yake na mara kwa mara husafiri mataifa ya Asia kwa matibabu.

clouds stream