Wednesday 18 January 2017

Obama atoa msamaha wa mwisho kwa wanajeshi

Hii ni nafasi ya mwisho kwa Obama kabla ya kuondoka madarakani

Hii ni nafasi ya mwisho kwa Obama kabla ya kuondoka madarakani
img-20161130-wa0008

Rais Obama amebatilisha kifungo cha jela kwa Chelsea Manning, aliyekuwa mwanjeshi wa Marekani aliyehukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kufichua nyaraka za siri.

Taarifa kutoka ikulu zinasema Manning ataachiwa huru ifikapo mwezi wa tano.

Mwanajeshi huyo aliyekuwa mwanamageuzi alifanya kazi huko Iraq alikuwa akijulikana pia kama Bradley Manning.

Chelsea Manning awali alikana makosa yake kabla ya kukubali
Chelsea Manning awali alikana makosa yake kabla ya kukubali

Alikutwa na hatia hiyo mwaka 2013 kwa kuweka karibia robotatu ya mamilioni ya nyaraka za siri za kijeshi na kidiplomasia katika tovuti ya WikiLeaks.

Rais Obama pia ametoa msamaha kwa mstaafu Generali James Cartwright, aliyekubali kosa la kutoa taarifa za uongo katika uchunguzi uliokuwa ukifanywa na FBI katika udukuzi wa compyuta kuhusu mipango ya kinyuklia ya Iran.

clouds stream