Wednesday, 11 January 2017

BAADA YA SIMBA KUPATA USHINDI WA MATUTA DHIDI YA WATANI WATAWEZA KIUFUNGA AZAM ?

BUKUNGU
Basala Bukungu wa simba akishangilia bao alilo wa funga yanga.
img-20161130-wa0008

kufuatia ushindi wa mabao manne kwa sifuri ilioupata Azam fc dhidi ya Yannga katika hatua ya makundi ni dhahiri shahiri kwamba timu hiyo ipo katika kiwango kizuri ukilinganisha na Simba ambao waliibuka na ushindi wa penati dhidi ya Yanga.

Simba ambayo haikuonesha mchezo wa kulizisha hasa katika safu yake ya ushambuliaji katka mechi hiyo ya watani wajadi na hata ile ya URA walio toka bila kufungana hii inaonyesha  itawapa wakati mgumu pindi watakapo kutana na wana walambalamba hao walioifunga Yanga kwa kandanda safi na la uhakika.

Simba na Azam wanatarajia kucheza fainali ya mashindano hayo ya kuazimisha siku kuu ya mapinduzi ya Zanzibar inayo fanyika kila tarehe 12 January ya kila mwaka. Fainali itafanyika siku ya ijumaa 13/januari/ 2017.

clouds stream