Sunday 29 January 2017

Trump ajitetea kuhusu sera ya usafiri aliyoianzisha Ijumaa

Trump amekosolewa vikali kwa sera hiyo

Trump amekosolewa vikali kwa sera hiyo
img-20161130-wa0008

Rais wa Marekani Donald Trump ametetea marufuku yake ya muda ya kusafiri kwa watu wanaotoka katika nchi saba ambazo ni za kiislamu baada ya watu kuukosoa uamuzi huo huku wengine wakiandamana.

Katika taarifa ya maandishi, bwana Trump amevilaumu vyombo vya habari kwa kupotosha taarifa kwamba marufuku hiyo ni kwa waislamu.

Amesema viza zitatolewa kwa wasafiri kutoka nchi zote ndani ya siku tisini.

Katika hali inayoonekana kulegeza msimamo wa amri ya kiutendaji iliyopitishwa siku ya Ijumaa, Reince Priebus, ambae ni kiongozi wa wafanyakazi wa serikali amesema marufuku hiyo haitawahusu wenye kuhodhi kadi za green, ambao wana haki ya kisheria kuishi nchini Marekani.

Mhariri wa BBC kaskazini mwa marekani amesema ikulu ya marekani imekosolewa vikali kwa sera hiyo.

Mamia ya watu wameandamana kupinga hatua hiyo
Mamia ya watu wameandamana kupinga hatua hiyo

Wakati huo huo, maelfu ya waandamanaji wanaopinga amri hiyo ya Trump kwa mara nyengine wameandamana katika viwanja vya ndege na sehemu nyinginezo nchini Marekani.

Waandamanaji wamepita katika miji ya Boston, New York na karibu na ikulu mjini Washington.

Mwanasiasa mwandamizi wa Republican ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya senate ya mambo ya nje, Bob Corker, amesema amri hiyo ya Rais utekelezaji wake haukuwa na ufanisi,hivyo kutaka mabadiliko ya haraka kufanywa.

Washauri wakuu wa masuala ya sheria kutoka majimbo kumi na sita nchini Marekani wameshutumu marufuku hiyo ya kusafiri na kusema haiko kisheria, imekiuka maadili ya kimarekani na imekiuka katiba ya nchi.

Kwa upande wake, Hakeem Jeffries kutoka chama cha Demokrat, alikuwa ni miongoni mwa walioandamana katika uwanja wa ndege wa JFK mjini New York.

Amesema idadi kubwa ya watu wanazuiwa kinyume cha sheria katika uwanja wa ndege.

clouds stream