Donald Trump alikutana na wakuu wa ujasusi siku ya Ijumaa
Maafisa wa ujasusi wa Marekani wamemlaumu Rais Putni wa Urusi kwa kuamuru binafsi shughuli za udukuzi nchini Marekani kwa juhudi za kupendelea au kumsaidia Bwana Trump ashinde katika Uchaguzi wa Urais uliofanywa mwaka uliopita.
Ripoti iliyotolewa na maafisa hao ilisema kuwa Urusi ilikusudia kuchochea ili wananchi Wamarekani wakose imani katika katika demokrasia ya nchi yao na pia kumdhalalisha mpinzani wa Bwana Trump, Bi Hillary Clinton.
Ripoti hiyo kwa mara ya kwanza inamshirikisha Bwa Putni katika shughuli za udukuzi moja kwa moja katika uchaguzi wa Marekani.
Makamu wa Rais Mteule, Mike Pence, alisema baadaye kuwa Bwana Donald Trump baadaye atachukua hatua kali dhidi ya udukuzi wo wote unaokabili Marekani kutoka kwa taifa lo lote lile.
Baada ya kukutana na maafisa wa ujasusu, Bwana Trump alisema kuwa amejifunza mengi kuhusiana na shughuli za udukuzi lakini akakanusha kuwa udukuzi huo ulibadili mkondo wa matokeo ya uchaguzi wa Urais kwa njia ye yote.
Donald Trump alikuwa amedokeza kuboresha uhusiano na Vladimir Putin