Wednesday, 25 January 2017

Marekani kujenga ukuta mara moja kati yake na Mexico


Marekani kujenga ukuta kuidhibiti MexicoMarekani kujenga ukuta kuidhibiti Mexicoimg-20161130-wa0008

Rais wa Marekani Donald Trump amesema serikali yake itaanza mara moja kushughulikia ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi yake kubwa aliyoiweka wakati wa kampeni za uchaguzi.

Akizungumza na wafanyakazi wanaohusika na usalama wa taifa, Donald Trump amesema ukuta huo utazuia wahamiaji haramu na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, kwa kuongeza kuwa siku zao zimekwisha wao kuishi na kufanya uharibifu.

Amesisitiza kauli yake ya kutaka Mexico kulipia ukuta huo, licha ya Mexico kukataa kufanya hivyo.

Wakati Marekani ikiweka msimamo wake huo, serikali na raia wa Mexico nao wameingilia kati kutetea nchi yao.

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto naye anashinikizwa kufuta mkutano wake na Rais Trump unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Washngton, ikiwa kama ni kujibu uamuzi huo wa Marekani kujenga ukuta.

Meya wa mji wa Mexico City Miguel Espinosa amesema kujengwa kwa ukuta huo, Marekani itajitenga yenyewe sio tu na Mexico bali na Amerika ya kusini yote.

Wakati huohuo, Rais wa Marekani amesema kuwa ana amini kwamba njia ya mateso inayotumika kuwahoji washukiwa wa ugaidi inafanya kazi vilivyo.

Akihojiwa na kituo cha Televisheni cha ABC, amesema Marekani inapaswa kupambana kwa nguvu zote katika kujibu mateso yaliyofanywa na kundi la Islamic State kwenye eneo la mashariki ya kati.

Mtangulizi wake Rais Barack Obama alipiga marufuku njia hiyo ya kutumia maji kuwahoji washukiwa kutokana na kuleta mabishano, mbinu hiyo ilikuwa ikitumika wakati wa utawala wa George Bush.

clouds stream