Wednesday, 25 January 2017

Ghana, Misri zasonga mbele Afcon

Misri

Wachezaji wa Misri wakishangilia goli lililofungwa na Mohamed Salah
img-20161130-wa0008

Michezo miwili ya mwisho ya hatua ya makundi ya michuano ya Afcon 2017 imemalizika kwa Misri kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ghana na hivyo kuongoza kundi D kwa alama 7 huku Ghana wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6.

Bao la ushindi la mafarao wa Misri lilifugwa na nyota wao Mohamed Salah, katika dakika ya 11 ya mchezo kwa mkwaju mkali wa mpira wa kutenga uliokwenda moja kwa moja nyavuni.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo timu ya Uganda walitoshana nguvu na Mali kwa kufungana bao 1-1.

Michezo ya hatua ya robo fainali itaanza kuchezwa jumamosi ya terehe 28 kwa Burkina Faso kucheza na Tunisia huku Senega wakicheza na Cameroon.

Jumapili kutacheza michezo miwili ya robo fainali ya pili kwa DR Congo kuchuana na Ghana nao Misri wakipimana ubavu na Morroco.

clouds stream