Wednesday, 4 January 2017

Tottenham yaisimamisha Chelsea,yaichapa 2-0

Dele Alli alikuwa nyota wa mchezo

Dele Alli alikuwa nyota wa mchezo
img-20161130-wa0008

Tottenham imefutilia mbali ndoto ya Chelsea kutaka kuweka historia katika ligi kuu ya England kwa kushinda michezo 14 baada ya vinara hao kuchakazwa 2-0 White Hart Lane.

Spurs wamekwaa mpaka nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi baada ya Dele Alli kufunga magoli yote mawili kwa njia ya kichwa hii ikiwa ni mwishoni mwa kipindi cha kwanza na dakika ya 54.

Alli alifunga vyema kwa kupokea pasi safi kutoka kwa Christian Eriksen kwa magoli yote mawili.

Kabla ya kupoteza mchezo huu Chelsea walishinda michezo 13 mfululizo
Kabla ya kupoteza mchezo huu Chelsea walishinda michezo 13 mfululizo

Eden Hazard alikuwa na nafasi mbili za kuiokoa Chelsea lakini Spurs waliweza kufanikiwa kupata alama tatu muhimu na kuwaondoa majirani zao Arsenal katika nafasi ya nne.

clouds stream