Sunday, 29 January 2017

Liverpool kumsafirisha Mane kwa ndege ya kibinafsi

Sadio Mane ameifungia Livepool mabao 8 msimu huu

Sadio Mane ameifungia Livepool mabao 8 msimu huu
img-20161130-wa0008

Liverpool wamepanga kumsafirisha kwa ndege ya kibinafsi mshambuliaji Sadio Mane, kutoka michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Gabon, ili kumpa nafasi ya kushiriki mechi na viongozi wa Ligi Chelsea.

Mane atasafirishwa baada ya Senegal kupoteza tena kwa mabao 5-4 ilipocheza na Cameroon wakati wa mechi ya robo fainali siku ya Jumamosi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 24, alipoteza penalti muhimu wakati wa mechi hiyo.

Liverpool imeshinda mechi moja tu tangu aondoke kushiriki mechi za kimataifa.

Walishindwa na klabu ya zamani ya Mane kwenye kombe la EFL siku ya Jumatano na kuondolewa kutoka kombe la FA walipocheza na Wolves.

clouds stream