Tuesday, 28 February 2017

Mkuu wa majeshi afutwa kazi Gambia

Gambia

Mkuu wa majeshi Ousman Badjie afutwa kazi Gambia
img-20161130-wa0008

Rais wa Gambia Adama Barrow amemfuta kazi mkuu wa majeshi Jenerali Ousman Badjie.

Jenerali Badjie alitangaza utiifu wake kwa rais aliyeondoka madarakani Yahya Jammeh baada ya uchaguzi wa Disemba ulioleta vuta nikuvute.

Hata hivyo, chini ya amri yake, jeshi halikutoa msaada wowote pindi vikosi kutoka nchi za Afrika Magharibi vilipoingia nchini Gambia mwezi jana.

Vikosi hivyo vilifanikiwa katika kumshawishi bwana Jammeh kukubali kushindwa na kuondoka nchini.

Wapelelezi 4 wa Korea Kaskazini wahusishwa na kifo cha Kim Jong nam

Kim Jong nam

Kim Jong nam
img-20161130-wa0008

Kitengo cha ujasusi nchini Korea Kusini kinaamini kwamba washukiwa wanne wa Korea Kaskazini wanaohusishwa na kifo cha Kim Jong nam ni wapelelezi.

Ndugu huyo wa kambo wa rais wa Korea Kaskazini aliwekewa sumu katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur kulingana na maafisa wa polisi wa Malaysia.

Wanne kati ya washukiwa saba waliotajwa na serikali ya Malaysia wanafanya kazi katika wizara ya usalama ,na ujasusi kulingana na wabunge mjini Seoul.

Haijulikani ni akina nani kati yao wanaotafutwa na serikali ya Malaysia.

Bwana Kim alifariki wiki mbili baada ya wanawake wawili kumfuata katika uwanja huo wa ndege.

Wanne kati ya washukiwa saba waliotajwa na serikali ya Malaysia wanafanya kazi katika wizara ya usalama ,na ujasusi kulingana na wabunge mjini Seoul.
Wanne kati ya washukiwa saba waliotajwa na serikali ya Malaysia wanafanya kazi katika wizara ya usalama ,na ujasusi kulingana na wabunge mjini Seoul.

Wanasema walidhani walikuwa wanahusishwa kufanya filamu ya mzaha.

Bwana Kim alipakwa sumu kali ya kuua neva kwa jina VX na kufariki akiwa na uchungu mkali kati ya dakika 15-20, alisema waziri wa afya wa Malaysia siku ya Jumapili.

Maafisa wa polisi wa Malaysia walimkamata raia mmoja wa Korea Kaskazini kwa jina Ri Jong Chol siku chache baada ya mauaji hayo.

Watu wengine 6 kutoka Korea Kaskazini wametajwa kuwa washukiwa na wanasakwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo.

Mmiliki wa Samsung mahakamani kwa kutoa hongo

Mrithi wa Samsung ahstakiwa mahakamni kwa tuhuma za kutoa hongo ili kupata usaidizi serikalini

Mrithi wa Samsung ahstakiwa mahakamni kwa tuhuma za kutoa hongo ili kupata usaidizi serikalini
img-20161130-wa0008

Mrithi wa kampuni tajiri zaidi nchini Korea Kusini, Samsung, atafikishwa mahakamani kwa madai ya kutoa hongo na ubadhirifu wa pesa, katika sakata kubwa inayoendelea kutokota, ambayo pia imesababisha kutimuliwa kwa rais, Park Guen-hye.

Mwendesha mashtaka maalum amesema kwamba, Lee Jay-yong, pamoja na wakuu wengine wanne wa Samsung watashtakiwa.

Kampuni ya Samsung
Kampuni ya Samsung

Bwana Lee, aliyekamatwa mapema mwezi huu, anashtakiwa kwa madai ya kutoa hongo ya takriban dola milioni 40, kwa mshirika wa karibu wa rais wa zamani, ili kupata usaidizi wa kisiasa.

Saturday, 25 February 2017

Simba Yaitafuna Yanga 2-1, Kichuya Awa mwiba kwa wana jangwani

C5g1cFAWgAU91WU
img-20161130-wa0008

Kwa mara ya tatu mfululizo timu ya Simba inamaliza mchezo dhidi ya Yanga katika Ligi Kuu Bara huku ikiwa pungufu katika ‘Dar Derby’ ambapo leo wana msimbazi hao wameikazia msuli Yanga na kuifunga goli 2 kwa ­1.

Simba sasa imefanikiwa kuondoka na pointi 4 katika michezo yao miwili dhidi ya watani zao Yanga baada ya kutoka sare katika mechi ya mzunguko wa kwanza na sasa inaongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 5.

Yanga ndio waliotawala mchezo wa leo kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha kwanza huku wakiisumbua safu ya ulinzi ya Simba mara kadhaa hali iliyopelekea mabeki wa Simba kujikuta wakifanya makosa madogomadogo yaliyowaletea balaa.

Ilikuwa dakika ya sita ambapo Yanga kupitia kwa mshambuliaji wake Simon Msuva ilipeleka kilio kwa wana msimbazi baada ya kuipatia timu yake goli  kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Simba Novalty Lufunga kumchezea madhambi Obrey Chirwa katika eneo la hatari.

Bao hilo lilidumu hadi mapumziko ambako katika kipindi cha pili Simba waliweza kucharuka na kutaka kusawazisha bao hilo kwa udi na uvumba.Wasanii, Mwana FA na Ommy Dimpoz wakifatilia mpambano huo.

Wasanii, Mwana FA na Ommy Dimpoz wakifatilia mpambano huo.

Vuta nikuvute hiyo ilishuhudia beki wa Simba, Jean Bukungu akilambwa kadi nyekundu dakika ya 54 na Muamuzi, Mathew Akrama kutoka Mwanza baada ya kumshika shati Obrey Chirwa akiwa mlinzi wa mwisho na kuisababishia Simba kubaki pungufu kwa mara ya tatu mfululizo dhidi ya watani zao Yanga.

Lakini kama ambavyo waswahili husema ‘Historia huwa inajirudia,’ kwa mara ya pili mfululizo Simba wameweza kutoka nyuma na kusawazisha bao dhidi ya Yanga huku wakiwa pungufu baada ya Laudit Mavugo kutikisa nyavu za Jangwani dakika ya 66 kwa mpira wa kichwa akimalizia krosi safi kutoka kwa Ajib.

Zaidi pia waswahili wanasema ‘Mtembea bure si sawa na mkaa bure,’ na usemi huo ulidhihirishwa na Chiza Kichuya dakika ya 81 pale alipopiga shuti kali kutoka nje kidogo ya eneo la hatari na mpira kukwamia katika nyavu za lango la Yanga na kuipatia Simba bao la pili.

Hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika Simba imeondoka na pointi 3 muhimu na kuwaacha watani zao Yanga wakimuwazia Kichuya na wasijue la kumfanya.16996292_1396063963790927_3820016781787035723_n

Viongozi Wa Serikali, Siasa Walioshuhudia Mnyama Akiiua Yanga

C5haSBtXMAQoMGf
img-20161130-wa0008

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Siasa leo walikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia mpambano kati ya watani wa jadi Simba na Yanga katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ambapo mnyama Simba ameibuka kidedea kwa kuibamiza Yanga goli 2­1 licha ya kuwa pungufu kwa muda mrefu.

Viongozi hao ni pamoja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Jamal Malinzi na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete. C5haR9vXMAAn1pfC5haSBrWMAAeU16C5haSBrWQAIntRfC5haSBtXMAQoMGf

Wednesday, 22 February 2017

Sayari nyingine saba sawa na Dunia zagunduliwa

Sayari zingine saba zagunduliwa anga za mbali

Sayari zingine saba zagunduliwa anga za mbali
img-20161130-wa0008

Wataalamu wa masuala ya anga za juu wa Marekani wakishirikiana na wengine duniani, wamefanya ugunduzi mkubwa wa sayari saba zenye ukubwa sawa na wa Dunia ambazo zinaizunguka nyota mojawapo kama ilivyo kwa dunia kulizunguka jua.

Wanasayansi hao wa anga za mbali kutoka Marekani, Uingereza na Ubelgiji, wamebainisha kuwa sayari hizo saba walizozigundua zinaizunguka nyota ijulikanayo kwa jina la Trappist One.

Hata hivyo wanasayansi hao wamesisitiza kuwa kwa teknolojia iliyopo sasa inaweza kuwachukua maelfu ya miaka kuzifikia sayari hizo.

Thomas Zurbuchen kutoka shirika la NASA lenye makao yake makuu Washington nchini Marekani, amewaambia waandishi wa habari kuwa haya ni mafanikio hayo ni makubwa kisayansi na yanajibu maswali makubwa ya kisayansi

"Ugunduzi huu unatupatia vidokezo muhimu vya kuitafuta 'dunia ya pili', na kwamba sasa si jamba la kusema kama ingelikuwa hivi, bali sasa tunasema ni lini. Wanasayansi wanaamini kwamba takribani katika kila nyota moja kuna uwezekano wa kuwepo sayari moja. Chukulia sasa nyota tatu, nne, tano hadi saba, jiulize ni idadi ya dunia ngapi zilizopo pale,'' amesema Zurbuchen.

SayariHaki miliki ya pichaNATURE

Michael Gillion ni mmoja wa wanajopo hilo la wana sayansi kutoka chuo kikuu cha anasema sayari tatu kati ya hizo saba zilizogundiliwa zipo karibu na nyota hiyo na zina sifa tofauti.

"Inaonyesha kuwa sayari hizi tatu kati ya hizo saba zilizogunduliwa zipo katika ukanda unaoweza kuruhusu viumbe kuishi, kwani maji yanaweza kupatikana na maisha ya viumbe hai yanaweza kuendelea, chakushangaza zaidi ni kwamba maisha yanaweza kuwepo hata katika uso wa sayari hizo," amesema Gillion.

Ugunduzi huu unatajwa na wanasayansi hawa kuwa ni mafanikio makubwa na umewaingiza katika ukurasa mwingine na kubakiwa na swali moja tu kwamba ni lini watazifikia sayari hizo badala ya kujiuliza kuwa katika anga hillo kuna nini.

Poster
Nasa imetoa bango la "kusafiri" kwenda kwenye mfumo huo wa nyota

Hata kuzifikia sayari hizo ni mtihani mwingine wani umbali wake hata mwendokasi wa mwanga, unaoongoza hapa duniani kwenda kwa haraka, unaweza kuzifikia sayari hizo baada ya miaka 40.

Maalim Seif ‘Amganda’ Dk.Shein Angoke Madarakani

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.
img-20161130-wa0008

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amemshauri Rais Dk. Ali Mohammed Shein kuachia madaraka kabla ya kuondolewa kwa nguvu na jumuiya za kimataifa kwa kile alichodai alimshinda katika uchaguzi Mkuu Oktoba, mwaka 2015.

Maalim Seif alisema hayo wakati katika ziara yake ya wiki mbili kisiwani Pemba ya kujenga chama, kwenye ukumbi wa Dolfin Bopwe, ambapo Maalim Seif alimtaka Rais Shein kuachia madaraka kutokana na kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

”Kama hakubali kuondoka kwa hiari yake basi amuangalie mwenzake Yahya Jammehy wa Gambia alivyoondoka madarakani bila ya hiari yake,” .

Amesisitiza kuwa ana uhakika na ushahidi uliowazi kuwa alimshinda Dk.Shein, lakini alitumia nguvu ya majeshi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi, jambo ambalo halimo katika taratibu.

Katika hatua nyingine Maalim Seif amewataka wanachama wake kutokubali kufanywa Chombo cha machafuko hivyo aliwasihi wanachama wake utulivu kwani muda wa kukabidhiwa madaraka umefika.

Hadi sasa katika ziara yake Maalim Seif ameshafungua matawi 12 ya chama hicho kwa Mkoa wa kusini Pemba na sasa anaelekea Mkoa wa Kaskazini.

Ridhiwani Asema Haya Kuhusu Kuchunguzwa Madawa Ya Kulevya

Ridhiwani Kikwete
Ridhiwani Kikwete
img-20161130-wa0008

Sakata la madawa ya kulevya linaendelea kuchukua sura mpya siku hadi siku na sasa Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameibuka na kueleza ya moyoni mwake baada ya hapo jana gazeti moja la kila siku kuwa na kichwa cha habari ‘Ridhiwani achunguzwa’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mbunge huyo ameandika yafuatayo;

“Ni jambo jema na la faraja kubwa kwangu kama uchunguzi unafanywa, ni ukombozi kwangu, ukweli utajulikana kuwa ni uvumi tu usiokuwa na chembe ya ukweli”
“Ni maneno ya watu wasionitakia mema, sina la kuficha…sifanyi biashara hiyo haramu na wala sijawahi kufikiria kufanya…..ni bora kufa masikini kuliko kutafuta utajiri kwa njia hiyo.”
rrrrr

Friday, 17 February 2017

TFF Yaonya Mabango Ya Kashfa Yanga Ikiwakaribisha Wacomoro

YANGA-1
img-20161130-wa0008

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeonya mashabiki wa mpira wa miguu nchini kutokuingia uwanjani na mabango ya aina yoyote yenye ujumbe wa kuikashifu Serikali au uongozi wa Shirikisho hilo.

Onyo hilo limetolewa leo ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo wa Kimataifa wa Klabu Bingwa Afrika kati ya wenyeji Yanga na Ngaya ya Comoro.

TFF imesema kuwa litawatia nguvuni kwa mujibu wa sheria na taratibu mashabiki watakaoikashifu serikali ama uongozi wa shirikisho hilo kwa kuingia na mabango uwanjani yenye jumbe tofauti hapo kesho katika mchezo wa kimataifa wa klabu bingwa Afrika kati ya wenyeji, Yanga dhidi ya Ngaya ya Nchini Comoro.

Watumishi TRA Matatani Kwa Madawa Ya Kulevya


Kamishna Mkuu Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga.
Kamishna Mkuu Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga.
img-20161130-wa0008

Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inawashikilia watumishi wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuhusika kupitisha viuatilifu vya kutengeneza dawa za kulevya.

Kamishna wa Operesheni wa mamlaka hiyo, Mihayo Msikela amesema watumishi hao walishirikiana na wanaosafirisha dawa hizo kuzipitisha hapa nchini.

Amedai kuwa watumishi wengine wawili wanafuatiliwa nyendo zao kabla ya kutiwa nguvuni kwa ajili ya mahojiano.

Thursday, 16 February 2017

Manji Athibitika Kutumia Unga, Kupandishwa Kizimbani Leo

Yusuf-Manji-002
img-20161130-wa0008

Hatimaye imedhibitika kuwa Mwenyekiti wa Timu ya soka ya Yanga na Mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania Yusuph Manji anatumia madawa ya kulevya na leo atapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo akiwa pamoja na watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kwa sakata kama hilo.

Katika Kipindi cha michezo katika redio moja nchini Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amethibitisha kuwa vipimo vya Mkemia Mkuu wa Serikali alivyofanyiwa Manji vinaonyesha kuwa ni Mtumiaji wa Madawa ya kulevya (Hakuyataja aina yake) na kusisitiza kuwa leo mtuhumiwa huyo atapandishiwa kizimbani kujibu shitaka hilo.

Akielezea afya yake tangu alazwe Hospitali, Kamanda Sirro amesema kuwa mwenyekiti huyo wa yanga yuko vizuri na sasa ameruhusiwa kutoka Hospitalini na kurejeshwa mahabusu polisi kusubiri kupandishwa kizimbani.

Sirro amesema kuwa habari kamili kuhusu sakata hilo na watuhumiwa wengine wakiwemo wasanii waliokamatwa zitatolewa leo mbele ya wanahabari Jijini Dar es Salaam.

Manji Athibitika Kutumia Unga, Kupandishwa Kizimbani Leo

Yusuf-Manji-002
img-20161130-wa0008

Hatimaye imedhibitika kuwa Mwenyekiti wa Timu ya soka ya Yanga na Mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania Yusuph Manji anatumia madawa ya kulevya na leo atapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo akiwa pamoja na watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kwa sakata kama hilo.

Katika Kipindi cha michezo katika redio moja nchini Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amethibitisha kuwa vipimo vya Mkemia Mkuu wa Serikali alivyofanyiwa Manji vinaonyesha kuwa ni Mtumiaji wa Madawa ya kulevya (Hakuyataja aina yake) na kusisitiza kuwa leo mtuhumiwa huyo atapandishiwa kizimbani kujibu shitaka hilo.

Akielezea afya yake tangu alazwe Hospitali, Kamanda Sirro amesema kuwa mwenyekiti huyo wa yanga yuko vizuri na sasa ameruhusiwa kutoka Hospitalini na kurejeshwa mahabusu polisi kusubiri kupandishwa kizimbani.

Sirro amesema kuwa habari kamili kuhusu sakata hilo na watuhumiwa wengine wakiwemo wasanii waliokamatwa zitatolewa leo mbele ya wanahabari Jijini Dar es Salaam.

Diamond Platinumz Afafanua Sababu Za Kuitwa Na Kuripoti Polisi

C4tzofVWYAAtjVT
img-20161130-wa0008

Msanii, Diamond Platinumz amefafanua sababu za yeye kuripoti katika kituo cha polisi na kusema kuwa ilikuwa ni kwasababu ya uendeshaji mbaya wa gari huku kukiwa na picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikimuonesha yupo kituo cha polisi.

Diamond amethibitisha hilo kupitia Instagram yake kwa kuandika >> ‘picha hizo leo nilireport kituo kikuu cha polisi wa usalama barabarani kutokana na video clip tuliyopost naendesha gari barabarani bila kufunga mkanda na pia kuachia usukani na  kucheza‘

‘Nikapewa Onyo na kulipa faini kwa mujibu wa sheria… tafadhali watanzania na Vijana wenzangu… tuhakikishe tunafunga mikanda pindi tupandapo na tuendeshapo Magari Maana ni Hatari kwa Maisha yetu na inaweza kukupeleka kunyea debe.

 Kwa mujibu wa Diamond, amepewa onyo na kulipa faini kutokana na kosa hilo. Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani, Kamanda Mpinga alimuita msanii huyo kituo cha polisi baada ya kuona ‘clip’ hiyo.

Katika kipande hicho cha video, Diamond anaonekana akiwa na mpenzi wake Zari, mama yake pamoja na watoto ndani ya gari linaloendeshwa na Diamond wakisikiliza na kucheza nyimbo mpya ya Msanii huyo ya “Marry Me” aliomshirikisha staa wa Marekani, Neyo, na ndipo Platinumz anaachia usukani na kuungana na Zari katika kuserebuka mziki.

Ridhiwani Kikwete Atoa Ya Moyoni Sakata La ‘Unga’

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
img-20161130-wa0008

Sakata la Madawa ya kulevya lime endelea kuchukua mijadala hapa nchini ambapo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete ametoa ya moyoni kuhusiana na Sakata hilo.

Akizungumza katika maohojiano na moja ya redio jijini hapa Ridhiwani amesema kuwa serikali inatakiwa kuiendeleza vita ya Madawa ya kulevya kama ilivyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda hadi ifike mwisho na kuyatokomeza kabisa hapa nchini.

Amesema Madawa ya kulevya yamepoteza maisha ya vijana wengi wenye uwezo mkubwa na mchango katika taifa ambapo amemtolea mfano msanii kama Langa aliyefariki dunia pamoja na shida anazozipata mwanamuziki Ray C.

Ridhiwani amesema yeyote atakayethibitika kuhusika, achukuliwe hatua, huku akionesha imani kubwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Rogers William Sianga aliteuliwa hivi karibuni.

Kwa upande mwingine Ridhiwani amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuanzisha vita hiyo na kutaka wahusika wachukuliwe hatua kali.

Sunday, 12 February 2017

Korea Kaskazini kujadiliwa

Korea Kaskazini

Kombora la Korea Kaskazini
img-20161130-wa0008

Marekani, Japan na Korea ya Kusini wameomba kuwepo kwa mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ili kujadili jaribio la kombora la hivi karibuni lililofanywa na Korea ya Kaskazini katika bahari ya Japan.

Japan na Marekani zimelaani majaribio ya makombora ya masafa marefu yaliyofanywa na Korea Kaskazini katika bahari ya Japan.Rais Trump na kiongozi wa Japan, Shinzo Abe, walikuwa wanakutana mjini Florida pindi uzinduzi huo wa makomboro ulipofanyika.Bwana Abe amelielezea tukio hilo kuwa halivumiliki.

Kwa upande wake, Donald Trump amesema Marekani itashirikiana na Japan kwa asilimia mia moja.Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini nae, amesema jaribio hilo, ambalo linakiuka vikwazo vya umoja wa mataifa, linaonyesha azma ya Korea Kaskazini ya kukuza teknolojia ya makombora ya nuklia.

Raia huyu katika mji mkuu wa Korea Kaskazini wa Pyongyang, wanaonyesha jinsi wanavyounga mkono mpango wa kivita wa nchi yao, nchi yetu imeonyesha msimamo wake wazi, kwamba tutaendelea kujenga uwezo wetu wa kujilinda, kwa kutumia nguvu za nuklia, na uwezo wa kushambulia, katika kipindi ambacho maadui wetu wanaendelea na vikwazo vya kutugandamiza. Tutatetea amani na usalama wa nchi yetu kwa njia yoyote, kwa jitihada zetu wenyewe, na tutachangia amani ya dunia na utulivu."

Mshauri mwandamizi katika ikulu ya Marekani amesema serikali ya rais Trump ,itaimarisha ushirikiano muhimu katika eneo la pacific ili kuepusha hali ya uhasama kutoka Korea ya kaskazini.

Katika mahojiano ya televisheni, Stephen Miller amesema uhusiano mkubwa baina ya nchi mbili umeonyeshwa mwishoni mwa juma ambapo ziara ya waziri mkuu wa Japan kwa marekani, ambapo amekaa katika nyumba ya rais trump mjini Florida.

Manji Achukuliwa Na Gari La Wagonjwa Kutoka Central



16640658_1383442345053089_6024557385772552086_n
img-20161130-wa0008

Mfanyabiashara Yusuph Manji ameonekana akichukuliwa na gari la wagonjwa ‘ambulance’  kutoka Kituo cha Polisi Kati anaposhikilwa tangu siku ya Alhamisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara au utumiaji wa madawa ya kulevya.

Bado haijafamika hasa nini kimetokea kupelekea Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Yanga kuchukuliwa kituoni hapo na gari la wagonjwa.

Ndugu msomaji endelea kufatilia mtandao huu kujua undani wa tukio hili kadiri tutakavyopata habari kutoka mamlaka husika.

Manji ni mmoja wa watu 65 waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujihusisha na biashara ya mihadarati na alifika kituoni hapo siku ya Alhamisi pamoja na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye aliachiwa.

Hata hivyo, gari lake binafsi na lile la wagonjwa lililombeba yalionekana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili yakiwa yamesimama katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

JPM Awaapisha Makamishna Dawa Za Kulevya, Uhamiaji Na Mabalozi

16508005_1383276638402993_544378440421370196_n
img-20161130-wa0008

Rais, Dkt. John Pombe Magufuli  amemuapisha Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Madawa ya Kulevya na wasaidizi wake wawili.

Pia amewaapisha Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Jenerali Dkt. Anna Makalala na mabalozi watatu.

 Mabalozi hao ni Omary Yususph Mzee (Algeria), Joseph Sokoine (Ubelgiji) na Grace Mgovani (Uganda). 

Amemtaka Kamishna Mkuu wa kupambana na dawa za kulevya kufanya kazi bila kuogopa ili kuweza kuokoa nguvu kazi ya taifa inayoteketea.

Rais Magufuli akimuapisha Rodgers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Rais Magufuli akimuapisha Rodgers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Ameongeza kuwa vita dhid ya dawa hizo ni ngumu kwa sababu ina faida kubwa na hivyo wafanyabiashara wa dawa hizo wanaweza kufanya chocote kwa fedha zao na kuongeza kuwa kama isingekuwa sheria imesema yeye mwenyewe angekua mwenyekiti wa timu ya kupambana na dawa hizo.

‘They can do anything at any cost,’ lazima tushirikiane katika vita hii,” amesema Rais Magufuli.

Amemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na mabalozi katika nchi ambazo kuna watanzania wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya wasijihusishe katika kuwatetea wahalifu hao kwa namna yoyote ile na kuacha sheria zifuate mkondo wake.

Aidha, amewataka waandishi wa habari na wanamitandao kuweka Utanzania mbele na pale anapotokea mtu anapambana na dawa za kulevya wamuunge mkono badala ya kumchafua.

“Vita hii ya dawa ya kulevya ni kubwa sana na hatuwezi kwenda nayo kimzahamzaha na Serikali itahakikisha inasimamia vyema Sheria ya Mwaka 2015 ya Madawa ya Kulevya,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemtaka Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Idara ya Uhamiaji kutokana na utendaji kutoridhisha.

“Nataka ufanye mabadiliko makubwa Uhamiaji izalishe fedha, ukadhibiti utoaji ‘Passport’ maana zimekuwa zikitolewa kiholela,” amesema Rais Magufuli.

Thursday, 9 February 2017

Rais Kenyatta Azua Gumzo Kusakata Muziki Ikulu


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akisakata Muziki Ikulu.img-20161130-wa0008

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (Katikati) akisakata Muziki Ikulu. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezua gumzo kufuatia kucheza muziki alipokutana na kundi moja la wachezaji densi ndani ya mjengo wa Ikulu ya Nairobi siku ya Jumatano.

Kwenye mitandao ya kijamii Watu wamekuwa wakitumia #DabOfShame, kumkosoa rais huyo, wakisema analenga tu kuimarisha kampeini yake, ilihali taifa hilo liko katika lindi la matatizo chungu nzima, ikiwemo mgomo wa muda mrefu wa madaktari na wahudumu wa matibabu.

Hivi karibuni Rais Kenyatta amekuwa akikutana na watu mashuhuri na wasanii wa muziki, kusaidia mikakati yake ya kupata kura dhidi ya wapinzani wake.

Wafuasi wake wanasema kuwa, anaonesha kuwa ni mtu wa kufikiwa kwa urahisi. 

Trump Agonga Mwamba Mahakama Ya Rufaa, Aazimia Kupambana Na Mihadarati


Rais wa Marekani Donald Trump trump.
Rais wa Marekani Donald Trump trump.

img-20161130-wa0008

Mahakama ya Rufaa nchini Marekani imekataa kuirudisha tena marufuku iliyowekwa na Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kwa wasafiri kutoka nchi saba za Kiislamu na Wakimbizi wote kuingia nchini humo.

Jopo la Majaji watatu kwa kauli moja limekataa kuupindua uamuzi uliotolewa na Jaji kutoka Mji wa Seattle, ambaye wiki iliyopita alizuia sehemu za amri iliyotolewa na Rais huyo wa Marekani.

Habari zinasema kwamba uamuzi huo kwa sasa utapelekwa katika Mahakama ya Juu zaidi.

Na muda mfupi tu baada ya uamuzi huo wa mahakama kutangazwa, Rais Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba ana uhakika mwisho wake ataibuka mshindi.

 ”Ni uamuzi wa kisiasa na tutaenda kukutana mahakamani. Natarajia kufanya hivyo, tuna hali ambayo usalama wa nchi yetu uko hatarini na ni hali mbaya sana,” amesema Trump.

Katika hatua nyingine tena Rais Trump ametangaza mfululizo wa amri za Rais kwa lengo la kupunguza uhalifu.

Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo, Trump amesema uhalifu umeongezeka nchini Marekani na utawala wake utalishughulikia suala hilo kuanzia sasa.

Amri hizo zilizotangazwa ni pamoja na kukabiliana na magenge ya madawa ya kulevya na wafanyabiashara za kihalifu.

clouds stream